Zitto Kabwe ameitupia lawama manispaa ya Kinondoni pamoja na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kushindwa kudhibiti tatizo la uchafu katika fukwe za Coco Beach.
Amedai kuwa ni aibu kuwa manispaa hiyo inayoongozwa na chama cha upinzani ndani ya mkoa unaoongozwa na kijana, kushindwa kuhakikisha usafi katika fukwe hizo maarufu.
“Uchafu wa namna hii kwenye Manispaa inayoongozwa na Chama cha Upinzani ni aibu,” Zitto ameandika kwenye picha za fukwe hizo alizoweka kwenye mtandao wa Facebook.
“Lakini
ni aibu zaidi uchafu wa namna hii kuwa katika mkoa unaoongozwa Na Mkuu
wa Mkoa kijana katika mahala anapopita Kila Siku kwenda nyumbani kwake
Na kwenda kazini,” ameongeza.
“Hapa
Ni Coco Beach kwenye Mihogo. Hata sheria ndogo tu ya Manispaa ya
kuwataka wenye shughuli hapa kusafisha mbele ya eneo Lao ingeweka mahala
hapa kuwa safi. Kuna mambo hayahitaji misaada ya wazungu wala
Wafanyabiashara. Ni akili za kimaendeleo tu.”
Post your Comment