Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » Godbless Lema Akwama Tena Mahakamani Baada Ya Mawakili wa Serikali Kuweka Pingamizi .........Amerudishwa Rumande Hadi Disemba 2

Godbless Lema Akwama Tena Mahakamani Baada Ya Mawakili wa Serikali Kuweka Pingamizi .........Amerudishwa Rumande Hadi Disemba 2

Written By Bigie on Monday, November 28, 2016 | 3:27:00 PM

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema leo amefikishwa tena Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa ajili ya kusikiliza rufaa yake ya maombi ya dhamana.

Ulinzi ulikuwa umeimarishwa mahakamani hapo huku wafuasi wa Lema wakiwa  wamevaa fulana nyeupe zilizoandikwa Jutice 4 Lema mbele zikiwa na picha yake.

Mbele ya Jaji Fatma Masengi aliyekuwa  amepangwa kusikiliza Rufaa hiyo, Upande wa Jamhuri ambao ulikuwa ukiwakilishwa na mwanasheria Matenus J Marandu umeweka pingamizi kwamba mawakili wa Lema walipaswa kupeleka notisi ya rufaa kwanza na siyo kukata rufaa

Wakili wa Chadema Peter Kibatala amesema wao wameshakamilisha taratibu zote za kisheria, hivyo wanasubiri uamuzi wa pingamizi hilo lililowekwa na upande wa serikali.

Jaji Fatma Masengi ameutaka  upande wa serikali uwasilishe hoja za pingamizi lao  kwa njia ya maandishi kabla ya November 30 ili aweze kutolea uamuzi December 2 mwaka huu.
Ulinzi ukiwa umeimarishwa

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya