Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » Polisi Kutoa Taarifa Ya Kifo Cha Mwanamasumbwi Thomas Mashali Siku Ya Jumatano

Polisi Kutoa Taarifa Ya Kifo Cha Mwanamasumbwi Thomas Mashali Siku Ya Jumatano

Written By Bigie on Tuesday, November 1, 2016 | 10:01:00 AM

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa wanaendelea na upelelezi  kufuatia kuuawa kwa mwanamasumbwi Thomas Mashali na watatoa taarifa ya kifo hicho siku ya Jumatano.
 
Akizungumza na waandshi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro alisema taarifa zilizopo kufuatia kifo cha bondia huyo ni za kufikirika na zinasemwa tu, hivyo Jumatano atatoa taarifa hiyo.
 
Kamishina Sirro alisema kuwa bondia huyo ni mtu mkubwa na hakuna mtu aliethibitisha kuwa ni mny'ang'anyi, hivyo mpaka sasa ni maneno ya mtaani tu.
 
“Mimi ndio napata taarifa juu ya kifo cha bondia huyo. Ngoja nisubiri taarifa niweze kutoa siku ya Jumatano, ambapo nitakuwa na majibu sahihi. Kwa leo niache tu”alisema Kamishna Sirro.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya