Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 57 & 58 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 57 & 58 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Thursday, April 27, 2017 | 2:36:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
ILIPOISHIA
“Kusema kweli, ndani ya gari hatukukuta mwili wa mtu yoyote. Hata tulipo jaribu jaribu kutazama pembeni kuona kwamba labda mtu au watu walio kuwemo ndani ya gari hilo watakuwa wameangukia pembeni hatukuweza kuwapata”
“Unasema kweli?”
“Ndio Mrs Ranjiti, siwezi kukutania”
Kidogo hata nguvu za miguu zikamjia Phidaya, akajikongoja kongoja kwenda kuchungulia kwenye korongo hilo huku akiongozana na askari huyo sehemu alipo onyeshwa gari ilipo kutwa, alijikuta akitoa macho kwani ina umbali mrefu sana.
‘Sasa kama wametoka watakuwa wapi’
Phidaya aliiuliza huku akiendelea kuchhungulia chungulia bondeni kwenye korongo hilo.

ENDELEA
   Phidaya hakuhitaji kuondoka katika eneo hilo hadi apate ripoti ya mwisho kutoka kwa Polisi kwamba kijana wake Lee Si pamoja na Shamsa hawakuwemo kwenye ajali hiyo. Hadi yanatimu majira ya saa nne usiku, baridi ikiwa kali katika eneo la eneo hilo pamoja na ukungu mwingi, ulio tanda kila mahali hapakuweza kuonekana mtui wa aina yoyote aliye kuwamo kwenye ajali hiyo. Jambo hilo kwa upande mmoja liampa matumaini makubwa sana Phidaya. Akaagana na mkuu wa polisi aliye fika katika eneo hilo kushuhudia kazi ya vijana wake. Kwa usalama na kutona ni usiku sana, Phidaya akapewa gari mbili za polisi ziweze kuongozana naye hadi takapo fika mjini, gari mmoja ikatangulia mbele, huku ikiwa na askari wawili na gari moja ikafwatia kwa nyuma nayo ikiwa na askari wawili.
 
Safari yao haikukumbwa na tatizo la aina yoyote hadi walipo mfikisha Phidaya kwenye jumba lake la kifahari, lenye ulinzi madhubuti. Akaagana na askari hao wakimuahidi watampatia ripoti kwa kila jambo ambalo litatokea kwa wakati wowote katika uchunguzi wanao endelea kuufanya juu ya chanzo cha ajali hiyo. Mfanyakazi wake wa ndani, akampokea koti alilo livua na kulishika mkononi, taratibu Phidaya akangoza hadi kwenye meza ya chakula na kuketi.
 
“Dokta hajarudi?”
Phidaya alimuliza mfanyakazi wake wa ndani baada ya kukuta hapakuwa na chakula ambacho kimeweza kuguswa.
“Hajarudi bado”
“Hembu nitolee simu kwenye hilo koti langu”
Mfanyakazi wake akafanya kama alivyo agizwa, Phidaya akaipokea simu yake hiyo, kitu cha kwanza alipo minya batani ya kuwashia mwanga kwenye simu yake hiyo aina ya Iphone 6, akakutana na sura ya Black Shadow. Kwa haraka kumbukumbu zake zikarudi kwa mgonjwa huyo.
Akakurupuka kwenye kiti kama kichaa, hata kula hakutamani tena, akatoka nje na kuingia kwenye gari lake, walinzi wa getini wakamfungulia geti na kuondoka kwa mwendo wa kasi sana akiwahi hospital;ini.
                                                                                                               ***
    Majira ya saa tano kasoro usiku, Kim akiwa amevalia mavazi ya udaktari, pamoja na kitambaa cha kijani alicho jifunga puani na kuziba mdomo, huku kikiwa kimembakisha macho tu. Akaanza kutembea kuelekea kwenye kordo inayo kupeleka kwenye litio ya kushukia kwenye chumba cha siri.
Mavazi yote aliyo yavaa aliweza kukabidhiwa na dokta Yan. Huku dokta Ranjiti aki nje kabisa ya hospitali yake gari lake akiwa amelisimamisha sehemu ambayo anaweza kuliona geti la hospitalini kwake na endapo gari ya kubebea wagonjwa litatoka, basi ataungana nalo kuhakikisha kwamba Black Shadow wanamuua na kumzika.
 
   Hapakuwa na nesi wala mtu aliye weza kumstukia Kim, kutokana na jinsi alivyo vaa. Anaonekana kama daktari anaye toka katika chumba cha upasuaji. Kim akashuka na lifti hadi kwenye chumba ambacho amelazwa Black Shadow, akatembea kwa tahadhari kubwa hadi kwenye chumba ambacho ameelelezwa atamkuta Black Shadow.
Macho yake yakatua kitandani ambapo alitegemea kumkuta Black Shadow ila haikuwa hivyo kwani hakuwepo, kilicho bakishwa hapo ni kitanda na mashuka pekee. Akahisi labda amekosea, akatoka na kuanza kukagua vyumba vingine viwili, hakukuta kitu zaidi ya maboksi yenye dawa tu.
 
“Shitii…….”
Kim alizungumza kwa hasira huku akiitoa simu yake mfukoni akampigia dokta Ranjiti, hazikupita hata sekunde tano simu ikapokelewa.
“Vipi umefanikisha?”
Lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa dokta Ranjiti mara tu alipo pokea simu ya Kim.
“Mbona hayupo mgonjwa mwenyewe”
“Uuuu….unasem…aje?”
“Hayupo nimeingia kwenye chumba mulicho niagiza nimekumta hayupo”
 
Dokta Ranjiti hakuonge kitu chochote zaidi ya kukaa kimya, Kim akakata simu na kumpigia dokta Yan, naye akaonekana kushangazwa na taarifa hiyo, kutokana yeye yupo ndani ya hospitali kwa haraka akashuka hadi kwenye chumba, akadhibitisha kwamba Black Shadow hayupo. Kila mmoja akili yake ikajikuta akichanganyikiwa haswa dokta Yan, kwani kwa ugonjwa alio kuwa nao Black Shadow ni vigumu sana kwa yeye kuondoka hapo hospitalini na isitoshe amemchoma sindano ya usingizi inayo chukua masaa mengi sana hadi kuisha kwake mwilini.
                                                                                                       ***
    Dokta Ranjiti, akataka kuliwasha gari lake na kwenda hospitali ila alipo liona gari la Phidaya likiingia katika geti la hospitalini, akasitisha zoezi lake la kwenda hospitalini, kwa jinsi alivyo changanyikiwa akahisi akili yake ikitaka kupasua kichwa chake, japo ndani ya gari lake kuna hewa ya kiyoyozi, ila jasho lilimtiririka usoni mwake kama mtu aliye kimbia mbio ndefu.
 
Phidaya akasimamisha gari lake kwenye maegesho, kwa haraka akashuka na kuanza kutembea kwa mwendo wa kasi kuelekea ndani. Hakuhihitaji kusemeshana na mfanyakazi yoyote, akili yake kwa wakati huo inamfikiria Black Shadow tu. Akiwa kwenye kordo akapishana na Kim akiwa ameifunika sura yake, hakumtilia maanani sana. Akaingia kwenye chumba chenye lifti, akashuka chini, akaanzaa kukimbia hadi kwenye chumba alicho lazwa Black Shadow.
 
Macho na sura yake vikabadilika, gafla baada ya kukuta kitanda kikiwa hakina mgonjwa, dura ikajaa mikunjo, macho yakamtoka. Mwendo kasi ukaisha, akajikuta akianza kutembea kwa taratibu kukifwata kitanda hicho. Dokta Yan aliweza kumuona Phidaya akiingia ndani ya chumba alilichokuwa amelazwa Black Shadow, yeye akiwa kwenye moja ya stoo, mara baada ya Kim kuondoka, aliingia kutafuta tafuta, kwani naye akili yake ilichanganyikiwa. Kwa woga wa kumuogopa Phidaya akajibanza kwenye maboksi mengi ya dawa akihofia kuonekana kwa maana kesi nzima itamuangukia yeye.
 
Phidaya akajikuta akiishiwa nguvu za miguu na kujikalia kitandani, hakujua alie, acheke au afanye nini kwa wakati huo, akili yake ikakosa kabisa maamuzi ya kufanya hali ya hatari ikamjaa moyoni mwake. Taratibu akajikuta akilala chali kwenye kitanda hicho na kutazama feni lililopo juu kwenye chumba hicho linavyo zunguka taratibu taratibu.
                                                                                                             ***
   Kitendo cha gari kuanza kwenda chini, kwenye makorongo, Shamsa akaona kupiga kelele haita kuwa jambo la msaada kwao, kwa haraka akajirusha kwenye siti ya mwisho alipo Sa Yoo, anaye endelea kupayuka kwa makelele. Kutokana kioo cha nyuma cha gari hilo kimepasuka kikampa upenyo mzuri wa yeye kujitoa kwa haraka, akamshika mkono Sa Yoo, akamchomoa kupitia katika upenyo huo. Lee Si alipo ona juhudi za wasichana hao zimezaa matunda na yeye bila kusubiria gari kufika chini kabisa, akafungua mlango na kujitosha nje na kuanza kubingiria kwenye majani marefu. Sa Yoo na Shamsa nao waakendelea kubingiria kwenda chini wakiporomoka kwenye majani marefu. Cha kumshukuru Mungu Shamsa akabahatika kushikilia kijimti kilicho mzuia kwenda chini, hivyo hivyo ikawa kwa Sa Yoo. Kwa umahiri wa mazoezi aliyo nayo Lee Si, akafanikiwa kujizuia kwenye moja ya jiwe.
 
Mlipuko wa gari hilo, uliwastua kila mmoja wao. Kila mmoja aliweza kulishuhudia gari hilo likiteketea kwa moto, kutokana na nyasi nyingi zilizo kuwepo katika eneo hilo, adui yao Kim, hakuweza kuwaona kwa urahisi akaamini kwamba wameteketea  kwa moto. Wakasubira kwa muda hadi walipo sikia mngurumo wa gari la adui yao Kim lilipo ondoka ndipo na wao walipo anza kufanya jitihada za kupandisha kilima hicho.
 
 Haikuwachukua muda sana, wakafanikiwa kufika juu barabarani, wakaanza kutembea kwa miguu wakirudi kutokea mjini, kwa mwendo wa dakika tano, wakafanikiwa kusimamisha gari la mizigo, wakapewa lifti iliyo wafikisha hadi mjini kabisa. Muda wote walitembea kwa kujihami wakihofia kuonekana na adui yao kwani hawakutambua kwamba ni sehemu gani anapatika. Wakaelekea katika nyumba ambayo Sa Yoo, alikuwa akiishi na bibi yake, na baada ya msiba wa bibi yake aliicha na kwenda kuishi na rafiki yake Shamsa.
 
Kila mmoja akaanza kutibu majeraha ya mwilini mwake, hususani Sa Yoo, yeye ndio amepata mikwaruzo mingi sana, sehemu za mikononi na migongoni.
“Shamsa hivi umejifunzia wapi mbinu zote zile?”
Sa Yoo aliuliza huku akitabasamu, Shamsa, hakumjibu kitu chochote zaidi ya kutabasamu na yeye.
“Haki ya Mungu nilijua leo nakufa, yaani ahaa wee acha tu. Ila kusema kweli asante rafiki yangu Shamsa, kwa maana ningekuwa sasa hivi sijui nipo kuzimu au laa”
“Unapaswa kuwa mwana mazoezi”
“Na kamwili haka kweli nifanye mazoezi gani mimi?”
 
“Ya kujilinda”
Muda wote wa mazungumzo Lee Si hakuzungumza kitu chochote, aliendelea kusikilizia maumivu ya vidonda vyake. Hata wazo la kumpigia simu bosi wake kumpa taarifa kwamba wapo salama wala halikuwepo akilini mwake, aliendelea kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyo fanikiwa kutoka kwenye ajali hiyo.
Shamsa na Sa Yoo wakaandaa chakula, majira ya saa mbili usiku wote kwa pamoja wakajumuika mezani na kuanza kula.
“Wewe unaitwa nani?”
Sa Yoo, alimuuliza Lee Si, baada ya kumuona akiwa ametawaliwa na mawazo mengi kichwani mwake hata chakula hakukila kwa furaha.
 
”Lee Si”
“Asante pia kwa kutusaidia”
“Nanyi asanteni”
“Mimi naitwa Sa Yoo, huyu anaitwa Shamsa”
“Lee kwa nini uliamua kuhatarisha maisha yako na kutusaidia sisi”
Shamsa alimuuliza Lee Si.
“Ilikuwa ni moja ya kazi yangu niliyo weza kupewa na bosi wangu”
“Bosi wako ndio amekupa kazi ya kuhatarisha maisha yako?”
“Hapana bosi wangu aliweza kunipa kazi ya kukulinda wewe”
“Mimi…….!!”
Shamsa  alishangaa huku wakitazamana na Sa Yoo, kisha akamtazama Lee Si kwa macho hayo hayo ya mshangao
“Ndio bosi wangu ndiye aliye niagiza”
“Anaitwa nani?”
Sa Yoo alidakia mada
 
“Anaitwa Madam Phidaya mke wa Mr Ranjiti”
Shamsa akastuka kidogo, kijoko alicho kuwa akikipeleka mdomoni kikiwa na chakula akajikuta akikishusha taratibu na kukirudisha kwenye sahani yake.
“Laiti kama nisinge kulinda basi leo hii mungekuwa nyote walili maiti hususani wewe Shamsa”
Sa Yoo na yeye macho yakamtoka, kwa jinsi macho yake yalivyo na ukubwa fulani na yaduara, kwa jinsi yalivyo mtoka hadi Lee Si akacheka kidogo.
“Unacheke sisi kufa?”
Sa Yoo aliuliza kwa woga
“Hapana siwacheki, ila nimecheka kwa jinsi ulivyo yatoa macho yako”
“Sa Yoo una simu hapo?”
“Sina simu si tumeacha nyumba ile kule”
“Na wewe Lee Si”
 
“Sina nahisi simu yangu imeteketea kwenye moto kwa maana niliiangusha ndani ya gari”
“Kwani simu unaitaka ya nini na wewe?”
“Nahitaji tumpigie mama”
“Mama……!!”
“Ndio mama, Phidaya ni mama yangu”
Lee Si, habari aliyo isikia nayo ni mpya masikioni mwake,naye akajikuta akishangaa. Taratibu picha ya mazungumzo ya dokta Ranjiti na Kim ikaanza kumjia taratibu kichwani mwake.
“Sasa naanza kupata picha”
Lee Si alizungumza huku akitingisha kichwa chake
“Picha gani?”
“Mpango wote wa wewe kuuliwa ameupanga mume wake dokta Ranjiti?”
“What……?”(Nini…….?)
“Ndio, kitu kinacho takiwa kwa sasa hivi ni wewe kuwa makini kwani maisha yako yapo hatarini”
“Eheee hanijui huyu, ameingia pabaya”
Shamsa alizungumza huku akiacha kula na kunyanyuka, akaanza kutembea kwa haraka kuelekea nje, wezake nao wakamfwata huku Sa Yoo akimuita.
 
“Unakwenda wapi sasa?”
“Nakwenda kuonana na huyo Rnjiti”
“Nisikilize Shamsa, peke yako huwezi kupambana na Ranjiti, ni mtu mwenye pesa sana na endapo atakuona tena atakuua”
Lee Si alizungungumza huku akimzuia Shamsa aliye jawa na hasira, hakujua ni kwa nini daktari huyo anahitaji kumuu kwani hapakuwa na jambo lolote baya alilo weza kumfanyia daktari huyo. Lee Si akafanikiwa kumzuia Shamsa na kumrudisha ndani. Wote watatu wakakaa kwenye meza moja kwa mazungumzo zaidi.
 
“Kwa nini anataka kuniua”
“Nilisikia akizungumza na mtu aliye mpa hii kazi, kwamba wewe unatambua siri ya Phidaya”
“Siri…..! Siri gani?”
“Sijajua, ila nahisi kuna jambo ambalo Phidaya mwenyewe anahitaji kulitambua, ndio maana akaamua kukutafuta wewe ili uweze kumueleza ukweli”
Shamsa akashusha pumzi nyingi, kila kitu anacho kisikia kwa wakati huu kinamchanganya akili yake.
“Nahitaji kuonana na mama”
 
“Kwa leo itakuwa ni ngumu kuonana naye, kwa maana usiku huu atakuwa yupo nyumbani kwake”
“Kwani sasa hivi ni saa ngapi?”
Sa Yoo akasimama na kuingia kwenye chumba chake, akaitazama saa ya ukutani kisha akarudi sebleni
“Ni nne na dakika tano”
“Atakuwa amesha toka hospitalini”
Lee Si alisisitiza. Kutajwa kwa hospitalini, Shamsa akamkumbuka Black Shadow wake.
“Mungu wangu……!!”
“Nini?”
“Black Shadow lazima yule dokta atamuua, si anatambua kwamba yule ni mpenzi wangu, ili kuendelea kufivha mauvo yake atamuua tu”
 
“Ohooo sasa itakuwaje?”
“Itabidi twende hospitalini haraka”
Wote watatu wakakubaliana kwa pamoja wakatoka nje na kukodisha taksi, iliyo wapeleka hadi hospitalini. Taksi yao ikasimama pembeni na kulipisha gari la wagonjwa linalo toka kwenye hospitali hiyo, huku Kim akiwa ndio derava wa gari hilo, cha kumshukuru Mungu hapakuwa na mtu aliye weza kulifwatilia gari hilo la wagonjwa wala Kim, kuifwatilia taksi hiyo kwani Kim moyoni mwake amejawa na hasira sana, kwani kazi yake haijakwenda kama alivyo kusudia. Gari hilo lilipo toka taksi nayo ikaruhusiwa kuingia, moja kwa moja ikaenda kusimama kwenye maegesho ya magari. Lee Si akatoa waleti yake, mfuko wa nyuma wa jinzi alilo vaa. Akampa dereva taksi kiasi anacho wadai, kisha akashuka kwenye taksi, akiwa eneo hilo akaliona gari la Phidaya likiwa kwenye maegesho yake ya kila siku.
“Madam yupo ndani, gari yake hiyo hapo”
Lee Si alizungumza huku akianza kutembea kwa hatua ndefu kuelekea ndani ya hospitali huku akifwatwa nyuma na Sa Yoo na Shamsa. 
 
“Ohoo mjukuu wangu Lee Si mbona umeadimika siku hizi upo wapi?”
Bibi Eyna, alizungumza huku akiweka ndoo yake na ufagio wake wa kusafishia sakafu chini. Akamkumbatia Lee Si, kijana anaye mchukulia kama mjukuu wake.
“Nipo bibi, madam alinipa kazi kidogo nikawa nimebanwa banwa”
“Mbona umechubuka chubuka, alafu ni nyote watatu mumepatwa na nini?”
“Ahaa bibi nitakuambia badaye, vipi madam Phidaya yupo ofisini kwake?”
“Hapana nilimuona kwenye kordo akielekea chumba cha siri huko chini”
 
Bibi huyo alizungumza kwa sauti ya chini chini asisikike
“Kipo wapi hicho chumba?”
“Mmmm unataka kwenda kufanyaje?”
“Bibi ni historia ndefu ila nipeleke kwenye hicho chumba alafu mambo mengine yatafwata baadaye”
Kutokana bibi huyo anamuamini sana Lee Si akakubaliana naye, wakaongozana hadi kwenye mlango wa chumba chenye lifti ya kushuka chini kwenye chumba cha siri.
“Na hawa wanakwenda?”
“Ndio bibi niwageni wake”
“Nakuomba usinitaje Lee Si nisije nikafukuzwa kazi mie”
“Huwezi bibi Eyna kufukuzwa mimi nipo”
 
Bibi huyo akatazama pande zote za kordo hapakuwa na mtu akawaruhusu vijana hao kuingia kisha yeye akajifanya kama anafagia fagia maeneo hayo. Lee Si, Shamsa na Sa Yoo, wakashuka hadi chini kabisa kwenye chumba kwa kutumia lifti. Wakaanza kushangaa shangaa kwani ndani ya chumba hicho kuna taa nyingi na kiyoyozi kikali kidogo. Milango mitatu iliyopo mbele yao kidogo ikawapa utata wa kujua ni chumba gani wanapaswa kuingia. Ila kuna chumba amacho waliona mlango wake umerudishiwa. Wakapiga hatua hadi kwenye mlango huo, Lee Si, akausukuma kidogo ndani, na kuchungulia, akamkuta Madam Phidaya akiwa amejilaza juu ya kitanda. 
 
“Yupo huku”
Wote wakaingia na kumfanya Phidaya akurupuke kitandani na kukaa kitako. Phidaya hakuamiani macho yake alipo muona Shamsa na wezake. Kwa haraka akanyanyuka na kumkimbilia Shamsa wakakumbatiana. Phidaya akajikuta akiangua kilio kilicho mfanya hata Shamsa mwenyewe kulia.
“Mama”
Shamsa aliita kwa unyonge, taratibu Phidaya akamuachia Shamsa na kumtazama usoni akiwa haamini jina alilo itwa kwa haraka akamshika mkono, wakaka kitandani.
“Shamsa niambie unakumbuka nini kuhusu mim?”
Phidaya alizungumza huku akilia kwa uchungu
“Wewe ni mama yangu”
 
“Kweli……?”
“Ndio mama”
Phidaya akajipapasa kwa haraka, hakuiona simu yake, akanyanyuka na kukuta akiwa ameikalia, akaingia upande wa kuhifadhia picha na kuitafuta picha ya Black Shadow aliyo mpiga akiwa hana kinyago.
“Huyu je ni nani?”
Phidaya alizungumza huku machozi yakiendelea kumtiririka, Shamsa alipo ishika simu na kuiona picha ya Eddy akastuka, kidogo kwa sekunde kadhaa akaikuta akiwa kimya.
“Niambie Shamsa mwanangu, huyo ni nani?”
“Huyu ni baba. Baba Eddy”
Shamsa alizungumza huku machozi yakimwagika. Phidaya akaachia ukunga ulio mfanya Shamsa kumkumbatia kwa haraka na kuanza kumbembeleza.
 
“Wamemumua baba yako”
Phidaya alizungumza huku akiwa emekumbatiwa.
“Kina nani hao mama”
“Ranjti na wezake, ndio wamemuua. Baada ya kugundua kwamba Black Shadow ni mume wangu”
“Eheeeeeeeeee…….!!!!”
Shamsa alijikuta akimuachia Phidaya na kusimama huku akimtazama kwa mshangao, Lee Si na Sa Yoo nao wakabaki na mshangao kuyasikia maneno hayo.
“Ndio Black Shadow ndio huyo baba yako Eddy”
                                                                                   
SORRY MADAM (58)  (Destination of my enemies)

   Shamsa akajihisi kama nguvu zikimuishia, taratibu akarudi kitandani na kuketi pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote. Kila mmoja akabaki kimya, wakikosa kitu cha kuzungumza. Maumivu makali ya mapenzi yakamtawala Shamsa moyoni mwake, hakuamini asilimi kwamba Eddy ndio Black Shadow. Yote nikutokana na mapenzi mazito aliyo kuwa nayo kwa mpiganaji huyo.
 
“Mama sio kweli, Black Shadow hawezi kuwa baba”
Maneno ya Shamsa yalimshangaza kila mmoja wao. Mambo yate yakiwa yanaendelea dokta Yan aliweza kuwaona, kwa tahadhari kubwa akaanza kutoka kwa kunyata huku mwili mzima ukimtetemeka akafanikiwa kufika kwenye lifti pasipo kuonewa na mtu yoyote, akaingia na kupanda juu. Kitendo cha kutoka katika chumba hicho akakutana na bibi Eyna. Hakumsemesha kitu cha aina yoyote zaidi ya kumpita kama hajamuona. Akingia ofisini kwake na kujifungia kwa ndani, kwa haraka akachukua simu yake na kumpigia dokta Ranjiti.
                                                                                                      ***
  Dokta Ranjiti akiwa barabarani ndani ya gari lake huku akiongozana na gari ya wagonjwa inayo endeshwa na Kim wakielekea kwenye karakana yake, simu yake ikaita. Taratibu akaitoa mfukoni mwake, alipo kuta ni dokta Yan akaipokea na kuiweka sikioni.
“Dokta mbona yule msichana hajakufa?”
“Msichana gani?”
“Yule mtoto wa Phidaya”
“Unataka kuniambia Shamsa yupo hai?”
“Ndio nimemuona akiwa na yule binti aliye kuja naye ofisini kwako siku ile”
Akili ya dokta Ranjiti ikazidi kuchanganyikiwa, kila taarifa anayo ipata kwa sasa ni mbaya zaidi ya ubaya
                                                                                                       ***
  Kampeni za vyama vya upinzani na chama tawala nchini Tanzania, vikazidi kupamba moto. Mzee Godwin kila siku zilivyo zidi kwenda ndivyo jinsi alivyo zidi kupata umaarufu kwa wananchi wengi wa Tanzania. Maneno yake matamu yakazidi kuwapagawisha wananchi wengi. Kadri siku zilivyo zidi kwenda ndivyo chama tawala kilivyo zidi kupoteza umaarufu wake. Mzee Godwin kwa pesa aliyo kuwa nayo aliweza kuteka sehemu muhimu zenye ushawishi mkubwa wa watu wakiwemo wasanii wa muziki pamoja na wasanii wa filamu.
 
  Siku zikazidi kukatika na kuyoyoma. Siku ambayo wananchi wengi waliweza kuisubiria kwa hamu kubwa ikawadia. Tarehe ishirini na tano ya mwenzi wa kumi, wananchi wengi katika maeneo mbalimbali ndani ya Tanzania, wakajitokeza katika vituo zaidi ya elfu tatu vya kupigia kura. 
 
Zoezi hilo lililo funguliwa saa kumi na mbili asubuhi wananchi wakaanza kuwapigia kura, madiwani, wabunge na raisi ambaye walihitaji kuweza kumsimamisha madarakani.
 
Masaa yalizidi kuyoyoma hadi saa kumi na mbili jioni, wananchi wengine wakaba bado hawajapiga kura, hii ni kutokana na wananchi wengi sana kujitokeza katika zoezi hilo. Tume ya taifa ikaongeza siku iliyo fwata yaani tarehe ishirini na sita, wananchi waendelea kupiga kura wale ambao walikosa kupiga kura katika siku ya kwanza. Usimamizi wa kura uakazidi kusimamiwa kikamilifu, kuhakikisha kwamba hakuna chama kinacho ingia katika kashfa ya kuiba kura.
 
Siku ya pili zoezi lilizidi kwenda vizuri kwenye vituo vyote vya nchini Tanzania. Zoezi la kuhesabu kura likaanza, kila kituo kikatuma hesabu katika tume kuu ya uchaguzi. Matokeo yote ya uraisi katika vituo vyote zaidi ya elfu tatu, yakahesabiwa. Mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbio, msimamizi mkuu wa tume ya uchaguzi bwana Lukas Barnaba. 

Kwani chama tawala kimetupwa mbali sana kwa kura zilizo pigwa na wananchi. Ubaya ni kwamba katika ukumbi wa kuhesabia kura hizo hapakuwa na mtu yoyote aliye ruhusiwa kuwa na simu kuhofia kuvujishwa kwa matokeo.
 
Majira ya saa nne asubuhi, waandishi wa habari wengi kutoka sehemu mbalimbali, waliweza kukusanyika katika katika viwanja vya tume ya taifa.  Kila jambo linalo endelea katika viwanja hivyo yalirushwa moja kwa moja kupitia vituo vya televishion na redio. Hata watu wanao miliki blog pamona na website zao, nao walijitahidi kurusha matukio yanayo endelea.
 
Viongozi wa vyama mbalimbali nao waliweza kukusanyika katika viwanja hivyo kushushudia tukio hilo, kila kiongozi aliye kuwa akigombania nafasi ya uraisi, mapigo yake ya moyo hayakuweza kutulia, kila walipo waona watumishi wa tume ya Taifa, baadhi yao hawakusita kuwauliza uliza kitu kinacho endelea. 

Hapakuwa na mtumishi wa tume ya taifa aliye weza kuto majibu ya kuelewaka kwa viongozi hao wapatao nane walio kuwa wakigombani uraisai. Mzee Godwin na raisi Praygod wao wenyewe tu ndio hawakuweza kuwauliza watumishi wa uma kwani wanajiamini sana, hii ni kutokanana vyama vyao kuweza kuwa na nguvu kuwa ya kisiasa kwa wananchi.
 
Wakati wa kutaja matokeo ukawadia, mkuu wa tume ya uchaguzi akasimama kwenye moja ya sehemu iliyo andaliwa kwa zoezi hilo maalumu kwa watanzania wote walio weza kupiga kura zao kuwachangua viongozi wao. Kila mtu macho na masikio yake aliyaweka tayari kwa kusikiliza majibu hayo. Ukimya mkubwa ukatawala karibia uwanja mzima. Mkuu wa tume ya uchaguzi bwana Lukas Barnaba akawatazama watu walio kusanyika hapo woga mwingi ukamuingia, macho yake alipo yakutanisha na raisi Praygod Makuya, ndivyo jinsi mapigo yake yalivyo kwenda kasi.
“Ndugu Watan…zania”
Bwana Barnaba alizungumza kwa sauti ya kukata katia, mwili ukazidi kumtetemeka gafla miguu yake ikaishiwa nguvu na kuanguka chini na kupoteza fahamu.
                                                                                                ***
    Phidaya akawaomba Shamsa watoke kwenye chumba hicho, wakarudi juu huku kila mmoja wao akiwa na mawazo mengi kichwani mwake. Swali kubwa ambalo linawachanganya hadi kwa wakati huu ni sehemu gani ambayo Black Shadow amekwenda. Kila mmoja alipelekea mawazo yake kwa dokta Ranjiti. 

Shamsa aliongoza hadi ofisini kwa dokta Ranjiti. Ofisini hakumkuta mtu yoyote, ikawalazimu kuondoka katika eneo la hospitalini majira ya saa nane usiku. Wakaelekea kwenye moja ya hoteli ambapo Phidaya aliweza kukodishia vyumba viwili kwa ajili wajifiche hapo kwa kipindi kirefu, hadi mambo yatakapo kuwa shwari. Kazi walivyo kuwa nayo kwa wakati huo ni kuhakikisha kwamba wanamtafuta Eddy, nchi nzima hadi wampate.
 
Phidaya akarudi nyumbani kwake, akiwa katika hali ya mawazo mengi sana, ukimya nyumbani kwake ulimuonyesha dokta Ranjiti hajarejea. Chuki yake juu ya dokta Ranjiti ilizidi kuongezeka kila anapo mkumbuka kwa tukio ambalo amemfanyia Shamsa na kumfanyia Black Shadow.
“Lazima naye nimuue”
Phidaya alizungumza huku akijitazama kwenye kioo cha chumbani kwake.
                                                                                                         ***
   Dokta Ranjiti na Kim walipo ingia kwenye karakana, dokta Kim akaonekana mwenye hasira kali, akamkata jicho kali Kim pale alipo shuka kwenye gari ya wagonjwa hadi Kim akahisi kuna jambo ambalo limetokea.
 
“Vipi dokta mbona hivy……..”
Ngumi nzito ikatua shavuni mwa Kim na kumfanya ayumbe kidogo, akamgeukia dokta Ranjiti kwa hasira, akataka ajibu shambulizi hilo ila akakumbuka kwamba mtu huyo ni bosi wake na ni mtu muhimu sana anaye msaidia katika kuiepuka mikono ya polisi kutokana na utaalamu wake wa kutengeneza sura bandia.
 
“Umesema umemuua yule msichana ilabado wapo hai ni ujinga gani ulio ufanya weweeee”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa kufoka sana, macho yalikmtoka, jasho lilimwagika kiasi cha kumfanya aifungua tai yake na kuitupiakando.
 
“Ila bosi wamekufa kwenye ajali ya gari?”
“Wewee acha upumbavuuuu. Ona ona hawa ni kina nani?”
Dokta Ranjiti akampa simu yake Kim, akaona video fupi ambayo Dokta Yan alimtumia baada ya kuichukua kwenye chumba cha ulinzi, iliyo rekodiwa na moja ya kamera za kuingila mapokezi. Kim hakuamini macho yake kwani video hiyo iliwaonyesha vijana wote watatu, Shamsa, Sa Yoo na Lee Si.
“Umefanya nini Kim, na mbaya wamekutana na Phidaya mke wangu sijui yaani itakuwaje”
Dokta Ranjiti alichanganyikiwa sana.
“Bosi nipe nafasi ya mwisho nitahakikisha ninawatoa dunia”
“Hakikisha unafanya hivyo”
“Sawa bosi”
 
Kim alizungumza na kuondoka eneo la karakana, akiwa amejawa na mawazo mengi kichwani mwake. Hakujua ni jinsi gani vijana wale watatu wamezeje kuokoka kwenye ajali ambayo aliishuhudia kwa macho yake. Moyoni mwake alianza kupata woga kuwaogopa vijana hao, ila kutokana ni kazi ambayo amepewa na inamuingizia pesa akaona ni lazima aifanya ili maisha yake yaweze kusonga mbele.
 
Dokta Ranjiti kwa woga alio kuwa nao dhidi ya mke wake akiamini kwamba atakuwa ameelezwa kila kitu na Shamsa, walivyo kutana, akaona ni vyema kuto rudi nyumbani usiku huo, akaingia kwenye moja ya ndege yake ya kifahari, yenye kitand kizuri. Akagiza mfanya kazi wake kumletea chakula, akala na kulala, wala hakukumbuka kuoga.
                                                                                                       ***
  Majira ya saa mbili asubuhi Sabogo na msaidizi wake wakafika hospitalini ili kumjulia hali Black Shadow, kwa bahati nzuri wakamkuta dokta Yan akiwa anatoka kwenye moja ya chumba kumtembelea mgonjwa wake. Wakasalimiana naye, na kumuomba kumuona mgonjwa. 
 
Dokta Yan, akashindwa hata kitu cha kuwajibu, wawasiwasi wake usoni uliwadhihirisha Sabogo na msaidizi wake kwamba kuna tatizo ambalo limetokea kwa Black Shadow.
“Vipi dokta mbona unawasiwasi mwingi?”
 
“Black Shadow amepotea jana hospitalini”
“Amepotea…….?”
“Ndio hata sisi hatujui amekwenda wapi”
“Kwa…kwa.ni alipata nafuu?”
“Ndio alipata nafuu, sasa ndio hivyo ametoweka na hadi sasa hivi hatutambui alipo”
Sabogo hakutaka kukubaliana na maneno ya daktari huyo, kwa urahisi kiasi hicho, bila idhini ya daktari akaongoza hadi kwenye chumba cha siri ambapo Black Shadow amelazwa. Kweli akakuta kitanda cha Eddy kikiwa hakina mtu. Akazidi kuchnganyikiwa.
 
“Bosi tunafanyaje sasa?”
“Turudi kambini”
Sabogo na msaidizi wake wakaondoka, wakarudi katika kambi yake iliyo na vijana wengi wa mtaani. Akaitisha kikao cha dharura. Akatoa agizo kwa vijana wake hao kuhakikisha kwamba wanamtafuta Black Shadow popote alipo kwa madai yake mbele ya vijana ni kwamba kuna mtu anahusika na upotevu wa Black Shadow.
Vijana wa Sabogo ambao wengi wao wanaitambua sura halisi ya Black Shadow, wakaingia mitani na kuanza kufanya uchunguzi kuhakikisha wanampa mpiganaji wao.
                                                                                                               ***
    Hadi kuna pambazuka Shamsa hakupata lepe la usingizi, akilini mwake alizidi kumfikiria Black Shadow na Eddy. Moyoni mwake akazidi kujiaminisha kwamba hao ni watu wawili tofauti. Hisia zake za mapenzi juu ya Black Shadow, hakuhitaji kuzikatisha kiurahisi, kama alivyo sema Phidaya kwa maana anaamini kwamba Phidaya mwenye anahitaji msaada wake wa kuhakikisha kumbukumbu zake zinamrejea.
 
“Au sio Phidaya mwenyewe, mbona yule tulisha mzika?”
Shamsa alizidi kujiuliza maswali ambayo hakujua hata atajajibu vipi kwa maana hadi sasa hivi na yeye bado yupo njia panda.
“Umeamkaje?”
Sauti ya Sa Yoo aliye lala pembeni yake, ndio ilimstua kutoka kwenye dibwa la mawazo, akageuza kichwa chake taratibu na kumtazama Sa Yoo anaye piga miyayo ya usingizi.
“Nipo poa vipi wewe?”
“Safi, nimekusikia ukizungumza peke yako vipi kuna tatizo?”
“Kusema kweli Sa Yoo, hadi sasa hivi sijielewi kabisa. Sielewi jinsi mambo haya yanavyo kwenda kwenda”
 
“Huwelewi nini?”
“Jinsi Black Shadow, nilivyo ambiwa eti ni baba yangu. Pili ni kuhusiana na huyu mama yangu Phidaya, yaani nahisi kichwa changu kitanipasuka kwa mawazo”
“Unajua ni nini rafiki yangu Shamsa. Wewe ndio uliye baki katika huu mchezo, wewe ndio unaye takiwa kufumbua ukweli kuhusiana na familia yako”
“Nitaanzai wapi Sa Yoo, wakati mwanaume ninaye mpenda eti jana ninaambiwa kwamba ni baba yangu. Mama ambaye tulisha mzika leo yupo hai tena ni mke wa mtu maarufu hapa Japani, kweli niambie rafiki yangu mimi nitafanyaje?”
“Mmmmm, ni kweli mwanzo ni mgumu. Ila nina wazo?”
 
“Wazo gani?”
“Unaonaje ukajifanya wewe ni Black Shadow”
“Alafu…….?”
Shamsa alijibu huku akicheka
“Usinicheke Shamsa, wazo langu ni zuri sana”
“Ndio nalisikiliza sema mama.”
“Baada ya hapo unaanza kumtafuta dokta Ranjiti kimya kimya unambananisha. Ninaimani atakupa wewe ukweli tu”
“Kwa nini umeniambia mimi niwe Black Shadow na si wewe?”
“Hiii… kwani mimi najua hata kupigana. Fanya hivyo utafanikiwa rafiki yangu”
Shamsa hakuzungumza kitu zaidi ya kujilaza chali akitazama juu akilitafakari wazo la rafiki yake
                                                                                                           ***
   Wiki nzima ikakata pasipo Black Shadow kupatikana, Phidaya alijikuta akikonda taratibu kwani hofu yake yote ni juu ya mwanau ume huyo aliye elezwa kwamba ni mume wake. Hakujua ni lini alikuwa mume wake, ila kwa kauli za Shamsa aliweza kuamini maneno yake. Kila muda alijikuta akiitazama picha ya Eddy iliyopo kwenye simu yake. Mume wake aliye mpigia simu na kumueleza kwamba yupo Korea Kusini, kikazi, hakuhitaji kumfwatilia sana. Kwani alizidi kumchukia na endapo angemuona basi angemng’ofoa shingo yake.
 
   Hakupenda kukaa kabisa hospitalini kwake, mara nyingi aliweza kuutumia muda wake kwenda kutembelea sehemu mbalimbali zenye vivutio ili kupoteza mawazo yake. Siku ya leo aliamua kuutumia muda wake kwenda kwenye kituo kimoja cha watoto yatima. Akiwa na mlinzi wake Lee Si, walipeleka chakula pamoja na pesa nyingi katika kituo hicho ili kusaidia watoto hao wenye umri kuanzia mwaka mmoja hadi kumi na saba.
 
Macho ya Phidaya yakatua kwa mtoto mmoja, aliye jitahidi kukumbuka ni wapi alimuona, ila hakilini mwake hakuweza kupata kumbukumbu yoyote. Kwa ishara akamuita mtoto huyo ambaye kusema kweli amefanana sana na Junio, ila si Junio kwani huyu ni mdogo kwa Junio.
“Unaitwa nani?”
“Black Shadow….”
Jibu la mtoto huyo lilimfanya Phidaya kutabasamu huku akimtazama mtoto huyo.
“Unamua Black Shadow”
“Ndio namjuaa”
“Umemuona wapi?”
Kidogo mtoto huyo akasita, akamsogelea Phidaya sikioni na kumnong’oneza
 
“Nipe ela nitakuambia alipo Black Shadow”
Phidaya ikabidi acheke kidogo kwani mtoto huyo anaonekena ni mjanha sana.
“Una miaka mingapi?”
“Hiyoo”
Mtoto huyo alionyesha vidole vyake, vinne vya kiganja cha kulia. Phidaya akatoa noti ya dola mia na kumpa kijana huyo, kwa haraka kijana huyo akaificha pesa hiyo kwenye mfuko wake. Ili walezi wake wasioone kwani anaweza kupokonywa. Kutokana hawaruhusiwi kukaa na kiasi chochote cha pesa.
“Unataka kumuona…….?”
Mtoto huyo alizungumza kwa sauti ya chini hata Lee Si aliye simama pembeni hakusikia zaidi ya Phidaya peke yake.
“Ndio”
 
Phidaya naye alijibu kwa sauti ya chini kabisa. Mtoto huyo akamshika mkono Phidaya nakumnyanyaua kwenye kiti alicho kuwa amekaa.
“Lee Si nakuja”
“Sawa Madam”
Wakaongozana na mtoto huyo kuelekea kwenye mabweni wanayo ishi, walezi wakataka kuwafwata ila Phidaya akawazuia na kuwadanganya kwamba mtoto huyo anakwenda kumuonyesha bweni na kitanda anacho lala. Walezi hao wakaamini na kuwaacha waendelee na safari yao. Kweli wakaingia kwenye bweni lenye vitanda vingi, wakazidi kusonga mbele hadi kwenye vyoo vya ndani kwenye bweni hilo. Wakaingia kwenye moja ya choo.
“Yupo wapi huyo Black Shadow”
“Ngoja”
 
Mtoto huyo mwenye upeo mkubwa wa akili, kakapanda kwenye sinki la choo, ikabidi Phidaya amsaidie kupanda, kakaitoa picha iliyopo kwenye ikuta. Phidaya akaona shimo kwenye dogo kwenye ukuta huo. Mtoto huyo akaingiza mkono wake ambao upo sawa sawa na shimo hiko. Kuna kitasa akavuta kwa ndani, Robo ya ukuta wa choo hicho ukafunguka, hadi Phidaya akaogopa.
“Twende yupo huku”
“Ngoja kwanza mbona kuna giza humo ndani”
Mtoto huyo kwa kumtoa hofu Phidaya akaingia, akamisha batani kwenye moja ya swichi. Sehemu ya ndani ikaonekana vizuri. Ngazi nyingi zilizo shuka chini, zilizidi kumshangaza Phidaya. Taratibu akapiga hatua za uwoga, akaingia, ndani, mtoto huyo akaufunga mlango huo ulio kaa kama ukuta.
“Umepajuaje huku?”
“Babu yangu ndio alinionyesha huku”
“Babu yako”
“Ndio.”
“Kwanza unaitwa nani?”
“Naitwa Soroo”
 
Walizidi kushuka chini, wakakuta kordo moja ndefu iliyo jaa taa pembeni kwa juu,  mbele yake kwa mbali kuna mlango wa kuingilia kwenye chumba kimoja tu kilichopo kwenye eneo hilo. Wakazidi kupiga hatua, wakiwa umbali fulani kutoka kilipo chumba hicho, taa zikaanza kufifia. Wote wakajikuta wakiogopa, gafla taa zote zikazima na kujikuta wakipiga kelele za woga kwani giza zito lilitanda kwenye mboni za macho yao.

 ==>ITAENDELEA...

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com     

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts