Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » ALICHOSEMA FREEMAN MBOWE KUHUSU ISHU YA SHIBUDA.

ALICHOSEMA FREEMAN MBOWE KUHUSU ISHU YA SHIBUDA.

Written By mpekuaji on Wednesday, May 23, 2012 | 4:43:00 AM

Baada ya stori za mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda wa Chadema kupewa uzito sana kwenye vichwa vya habari vya magazeti, Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amezungumza Exclusive na Clouds Media Gruop kuhusu hiyo ishu.

Amesema “vyama vya siasa ni mjumuiko wa watu wengi, wenye uelewa na uvumilivu tofauti hivyo kutofautiana katika vyama vya siasa ni hulka ya kawaida na ni sehemu ya mchakato wa kujenga demokrasia”

Kwenye sentensi nyingine amesema “kwa mantiki hiyo ishu ya Shibuda tutaifanyia kazi kwenye utaratibu tu wa kawaida wa chama, hatuwezi kutoka kwenye track ya kufikiria mambo ya msingi kwa taifa alafu tukaanza kufikiria tofauti za mitizamo kati ya kitengo cha vijana na viongozi mmoja wapo, tutalimaliza kwa wakati, sioni kama linaweza kuathiri chama kwa njia yoyote ile kwa sababu halijagusa misingi ya uwepo wa chama.

Hili ni gazeti la Alhamisi May 17 2012.
Chama cha Chadema kitafanya mkutano mkubwa Dar es salaam May 26 kuhamasisha wananchi kujitokeza na kuijadili katiba ya taifa ili kufahamu serikali inakosea wapi na hatimae kuleta mabadiliko yanayotakiwa, Mwenyekiti Freeman Mbowe ameyazungumza hayo wakati alipotembelea makao makuu ya Clouds Media Group.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts