Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » LIVE!!! FUMANIZI LA WACHAWI WAKIWA KATIKA KANISA LA UFUNUO

LIVE!!! FUMANIZI LA WACHAWI WAKIWA KATIKA KANISA LA UFUNUO

Written By mpekuaji on Monday, May 21, 2012 | 8:56:00 AM

Watu hao wawili ambao ni Masaganya Kalimanzila umri wa miaka 30 (mwanamke) na Chiza Juma (mwanaume) waliotambulika kuwa ni wachawi mara baada ya kubanwa na kujitambulisha wamekamatwa majira ya saa 12 jana asubuhi katika kanisa la Ufunuo lililopo maeneo ya Butimba jijini Mwanza wakisafiri kwa ungo toka kijiji cha Kaziramkunda wilayani Kasulu mkoani Kigoma hadi jijini Mwanza kwania ya kuwachukuwa watu watatu walioagizwa kwaajili ya sadaka.


Kwa mujibu wa mahojiano waliyofanya na blogu hii wachawi hao wanasema kuwa walipewa amri na wakuu wao wanao ishi chini ya maji kuwachukuwa watu watatu wa kanisa hilo kwa mazingira ya kichawi ili wawauwe kwaajili ya kafara na mazindiko.


Pembejeo za kichawi mwanamke alisafiri kwa kutumia ungo na mwanaume akatumia mkuki na pembe.

Wananchi na baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi Mwanza wakiwa wamewazingira wachawi hao katika viwanja vya polisi Mwanza jana  asubuhi katika kuchukuwa maelezo.



Mchungaji wa kanisa la Ufunua Diana Bandele (kushoto) na Abigaili Zumaridi ambaye ni nabii wa kanisa hilo ambao waliwakuta wachawi hao kanisani mwao majira ya saa 12 kwani muda huo ni ada kwa wao kujitakasa kwaajili ya kuianza siku ya ibada.

Ingawa jeshi la polisi linaendelea kuchunguza juu ya hali hiyo, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuna kipengele kinacho utambua uchawi hivyo hakuna kesi inayowakabili watu hao.


watuhumiwa wa uchawi mwanza

Watu wawili waliotambulika kwa majina ya Masaganya Kalimanzila (mwanamke, miaka 30) na Chiza Juma (mwanaume) wakihusishwa na imani za uchawi baada ya kubanwa na wananchi, wamekamatwa majira ya saa 12 jana asubuhi  katika Kanisa la Ufunuo lililopo maeneo ya Butimba jijini Mwanza wakisafiri kwa ungo (mwanamke) na mshale (mwanaume) kutoka kijiji cha Kaziramkunda, Wilayani Kasulu, Mkoani Kigoma hadi jijini Mwanza, kwa nia ya kuwachukuwa watu watatu walioagizwa. 

Picture

hizi ni video za tukio zima


hizi ni video za tukio zima

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts