| SHIBUDA |
MBUNGE wa Maswa Magharibi kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Magalle Shibuda, ameendelea kusisitiza nia na msimamo wake wa kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.
Amewaomba kwa dhati wanachama wenzake wa CHADEMA kumwunga mkono katika nia yake hiyo na pia katika harakati zake za kukosoa tabia hasi ya baadhi ya viongozi wa chama hicho ya kuwanyima wanachama uhuru wa kutoa maoni kinyume na matakwa ya demokrasia.
Aliyasema hayo juzi wakati akiongea na waandishi wa habari mjini Shinyanga waliotaka kufahamu mustakabali wake na CHADEMA kufuatia tangazo lake la nia ya kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho lililozua mlolongo wa lawama kutoka kwa baadhi ya viongozi hususan Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) Bw. Ezekiel Wenje.
"Nasisitiza nia yangu kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama changu cha CHADEMA katikas uchaguzi mkuu ujao", alisisitiza nia yake.
Shibuda alisema tatizo lililopo na linalozidi kupanuka katika chama hicho ni baadhi ya wanachama na viongozi kuwa na fikra hafifu na kutokuheshimu demokrasia katika vyama vya kisiasa
Post your Comment


