Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » UBALOZI WA COMORO WATUMIWA KUTAPELI FEDHA

UBALOZI WA COMORO WATUMIWA KUTAPELI FEDHA

Written By mpekuaji on Tuesday, May 29, 2012 | 10:31:00 AM

Happy Dadson Gama.
Na Makongoro Oging'
UBALOZI wa Comoro nchini Tanzania unatuhumiwa kutumiwa kutapeli kampuni inayojishughulisha na utoaji wa mkopo iitwayo Enterprises Finance Limited (EFL).


Chanzo chetu cha habari ndani ya ubalozi huo kimedai kuwa, ofisa mmoja anahusika na utoaji wa barua na vitambulisho kwa wajanja kuonyesha ni wafanyakazi wao ili wapatiwe fedha kwa urahisi kutoka kampuni mbalimbali za mikopo. 


Mkurugenzi wa kampuni ya EFL, Jacqueline Lujuo alipoulizwa juu ya madai hayo alikiri na kueleza kuwa, mwaka jana dada aitwaye Happy Dadson Gama alifika ofisini kwao akiwa na barua iliyomtambulisha kuwa ni mfanyakazi wa Ubalozi wa Comoro ili apatiwe mkopo. 


“Nilipoona vielelezo, vitambulisho na barua niliamini kuwa ni mfanyakazi wa ubalozi huo, hivyo tulimpa mkopo wa shilingi milioni mbili,” alisema Lujuo.


Aliongeza kuwa, alishituka pale alipoona muda wa kurejesha mkopo umepita na Happy haonekani wala hatoi taarifa yoyote.
“Nililazimika kwenda kutoa taarifa juu yake katika Kituo cha Polisi Oysterbay na walipofuatilia hadi ubalozini waliambiwa mtu huyo (Happy) hawamfahamu na siyo mfanyakazi wao,” alisema Lujuo.


Alidai kuwa ilibidi katibu muhtasi wa ubalozi huo (jina tunalihifadhi) akamatwe kwa kudaiwa kushirikiana na Happy katika kughushi nyaraka za ofisi ikiwemo barua yenye kumbukumbu CMR/IF/OO/11 ya Agosti 19, mwaka jana na alimpa slip salary kuonesha kuwa mtuhumiwa alikuwa akipokea mshahara wakati siyo kweli.


Mwandishi wetu alipozungumza na katibu muhtasi huyo kwa njia ya simu alikiri kukamatwa na polisi kuhusiana na tukio hilo, hata hivyo alikata simu bila kutoa ufafanuzi zaidi.


Balozi wa Comoro nchini, Islam Balhabou hakupatikana lakini Mkuu wa Itifaki Ubalozini hapo, Dadson Gama ambaye ndiye baba wa Happy alipoulizwa kwa njia ya simu alisema mwanaye hana kosa lolote.


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, John Mtalimbo alipoulizwa kuhusiana na sakata hilo alisema analifanyia kazi.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts