Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , » UDSM WAMPA SIKU 15 WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

UDSM WAMPA SIKU 15 WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

Written By mpekuaji on Thursday, May 17, 2012 | 9:16:00 AM

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa 

KAMATI ya Elimu ya Juu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) imetoa siku 15 kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa, kutoa ufafanuzi kuhusu masomo yaliyopewa vipaumbele na yaliyonyimwa ili kuwawezesha wanafumzi kuomba kozi wanazozitaka na kuridhisha umma kuwa taifa limefikia kiwango hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati hiyo Fahami Mastawily, alisema bodi ya mikopo imetangaza sera mpya ya utoaji mikopo kwa kozi ambazo serikali imezipa kipaumbele hivyo wanahitaji waziri kutangaza rasmi masomo hayo.

Alisema vyuo vikuu 65 viko katika bodi ya mikopo ambapo jumla ya kozi 572 kati ya hizo 196 tu ndizo zimepewa kipaumbele na serikali, jambo alilosema si sahihi kwa sababu nchi bado ni maskini na changa, hivyo inahitaji wataalamu wa fani mbalimbali ili kukuza uchumi wa nchi.

Alidai uamuzi huo wa serikali kukiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 11 sehemu ndogo ya 2 na 3 inayosema kuwa kila mtu anayo haki ya kujielimisha na kila raia atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake.

Alisema sera hiyo inapingana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa mwaka 2007 wakati akiongea na wanafunzi wa elimu ya juu katika ukumbi wa Nkrumah, aliposema kuwa hakuna mwanafunzi atakayeshindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya masharti ya bodi ya mikopo au kwa sababu ya umaskini.

“Hii ni mojawapo ya makosa makubwa sana kwa sababu juu ya nani anastahili kupewa mikopo maana yake bodi inakuja na kigezo chake ambacho binafsi ninaamini ni cha kibaguzi, hakina haki na hakiwatendei haki Watanzania wanaolipa kodi ambayo inatumika kugharamia elimu ya juu,” alisema Fahami.


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts