Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » UPDATE: MUDA MFUPI UJAO TUTAKULETEA MWENDELEZO WA KESI YA LULU MICHAEL

UPDATE: MUDA MFUPI UJAO TUTAKULETEA MWENDELEZO WA KESI YA LULU MICHAEL

Written By mpekuaji on Monday, May 7, 2012 | 10:06:00 AM


Lulu.
KESI ya mauaji inayomkabili msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo inatarajiwa kutajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mara ya mwisho kesi hiyo ilipofika kwa ajili ya kutajwa, Aprili 23, mwaka huu, mahakama hiyo ilifurika waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali na baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kusikiliza kesi hiyo.

Kufurika watu huko kuliwafanya askari magereza kujitahidi kuweka ulinzi pamoja na kumficha msanii huyo ili asipate usumbufu wowote, jambo lililoleta purukushani kubwa na kumbana sana Lulu, kitendo kilichomfanya kulia mahakamani wakati akiingizwa mahakamani.

Kwa sasa kesi hiyo haijaanza kusikilizwa na iko kwenye upelelezi. Lulu anatetewa na Kamishna wa Tume za Haki za Binadamu Joaquine De-Mello, mawakili wa kujitegemea Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala na Fulgence Masawe.

Lulu anakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba ambapo anadaiwa Aprili 7, mwaka huu eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam, alimuua Kanumba.
Msanii huyo anasota rumande kwa sababu kesi ya mauaji haina dhamana.


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts