Blog hii imepokea taarifa ya kusikitisha usiku huu kutoka vyanzo vyake vya kuaminika ikieleza kuwa kuna ajali mbaya ya barabarani imetokea jana jioni na kupelekea vijana watatu wa kitanzania, wakazi wa Arusha kupoteza maisha na wengine ambao idadi yao haijajulikana kujeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, ambazo bado hazijathibitishwa na Jeshi la Polisi, vijana hao wamepata ajali nchini Kenya wakiwa njiani kurejea Arusha kutokea Jijini Nairobi wakitumia gari binafsi.
Vijana waliotajwa kufariki katika ajali hiyo mbaya ni Faraj Haule ambae ni mtoto wa Mchungaji Marko Haule, wa Kanisa la EAGT Elerai, Arusha na Denis Ngalesoni ambae ni mtoto wa mmiliki wa shule ya Green Acres ya Jijini Arusha.
Mwingine ambae jina lake halijaweza kutambulika mapema, anaelezwa kuwa ni mtoto wa mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite, maarufu kwa jina la Sunda.
Blog hii inatoa salamu za pole kwa wafiwa, na kumuomba Mungu aziweke roho za marehemu hao mahali pema peponi, na kuwapatia nafuu ya kupona majeruhi wote!
Tunaendelea kufuatilia zaidi..
Blog hii inatoa salamu za pole kwa wafiwa, na kumuomba Mungu aziweke roho za marehemu hao mahali pema peponi, na kuwapatia nafuu ya kupona majeruhi wote!
Tunaendelea kufuatilia zaidi..
Post your Comment


