Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » Kongamano la UDSM kutambua mchango wa Profesa Goran Hyden lafana

Kongamano la UDSM kutambua mchango wa Profesa Goran Hyden lafana

Written By mpekuaji on Sunday, June 10, 2012 | 12:21:00 PM

 Mwanataaluma mkongwe Profesa Goran Hyden akijibu hoja na maswali mbalimbali yalitolewa na wahadhiri na wanataalumu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania jana mjini Dar es salaam wakati wa kongamano la siku moja la wanataaluma liloandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wa Profesa Goran Hyden alioutoa ndani na nje Tanzania kitaalumu.

 Waziri Mkuu Mstaafu wa Uganda Profesa Apollo Nsibambi (kulia) akichangia mada  wakati wa kongamano la siku moja la wanataalum lililoandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wa Profesa  Goran Hyden alioutoa ndani na nje Tanzania. Wengine ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yambesi(katikati) na Profesa Goran Hyden(kushoto)
 Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es  salaam Profesa Rwekaza Mukanda (kulia) akibadilishana mawazo na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uganda Profesa Apolo Nsibambi (katikati) na Balozi wa Zambia nchini Judith Kangoma( kushoto) jana mjini Dar es salaam wakati wa kongamano la siku moja la wanataalum liloandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wa Profesa  Goran Hyden alioutoa ndani na nje Tanzania
 Profesa Bernadeta Killian wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam akitoa mada  kuhusu kitabu cha Profesa Goran Hyden cha 'Beyond Ujamaa in Tanzania' wakati wa kongamano la siku moja la wanataalum lililoandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wake kitaalum.

Katibu Mkuu zamani wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Juma Mwapachu akichangia mada wakati wa kongamano la siku moja la wanataaluma lililoandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wa Profesa Goran Hyden alioutoa ndani na nje Tanzania.Kulia ni Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es  salaam Profesa Rwekaza Mukanda. Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts