Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » STAA WA BONGO MOVE ATOA SINGO ‘KUMDISS’ NEY

STAA WA BONGO MOVE ATOA SINGO ‘KUMDISS’ NEY

Written By mpekuaji on Friday, June 22, 2012 | 5:44:00 PM

Nyota kutoka tasnia ya filamu Bongo, Latifah Idabu ‘Badra’ ametoa ‘singo’  inayomchana  ‘live’ staa wa Bongo Fleva, Ney wa mitego (mbavu nene).

Akizungumza na mtandao huu muda mfupi uliopita  Badra amefunguka kuwa  ameamua kutengeneza ngoma hiyo kufuatia kauli chafu dhidi ya wasanii wa kike  aliyotowa Ney kwenye wimbo wake mpya wa hip hop  ujulikanao kama ‘Nasema nao’  unaotamba hivi sasa kwenye vituo mbalimbali  vya redio.

“Nimechukizwa mno na kitendo cha Ney kuimba kuwa  mastaa wa Bongo move ni makahaba , hawezi kusema hivyo na sisi tukaa kimya, ametushushia hadhi hasa ukizingatia sisi ni kioo cha jamii, ni zamu yake sasa  kusikia nilichomwambia na  kama kitamuuma  atajibu” alisema  Badra na kumalizia kwa tusi.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts