Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » Taarifa za TEF hazina ukweli; Sina ugomvi na Waziri wangu - Kamuhanda

Taarifa za TEF hazina ukweli; Sina ugomvi na Waziri wangu - Kamuhanda

Written By mpekuaji on Saturday, June 9, 2012 | 8:48:00 PM

Picture: Seth Kamuhanda na Mwembezi Gasper
Kamuhanda akizungumza katika mkutano na wanahabari, Dar es Salaam akikanusha habari zilizoandikwa kwenye vyombo habari kwamba haelewani na Waziri wake. Kulia kwake ni Gasper Mwembezi, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara hiyo. (picha: Richard Mwaikenda)
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imekanusha taarifa kuwa kuna msuguano kati ya Waziri na Katibu Mkuu katika Wizara hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Seth Kamuhanda wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari  jijini Dar es Salaam leo.

Alisema taarifa hizo zilizoandikwa na Jukwaa la wa Hariri Tanzania (TEF),  kwenye vyombo vya habari kuwa hazina ukweli wowote kwani viongozi hao wamekuwa na  ushirikiano mzuri  kati kazi hivyo si rahisi kutokea migongano kama ilivyodaiwa.

Kamuhanda alisema nawaomba wanahabari mkitoka hapa muwafikishiye taarifa hizi wananchi  kuwa katika Wizara hiyo hakuna migongano na wahakikishia kuwa haitatokea kwa kuwa hakuna tofauti yeyote kati yao.

"Unajua hali kama hiyo ya mimi kugongana na Waziri kwa kuwa kila mmoja wetu amekuwa akifanya kazi yake kwa uadilifu mkubwa hivyo basi, haitatokea hata siku moja kutokea tofauti."

Akizungumzia ni kwa nini walishindwa kufika siku ya kufungua na kufunga mkutano huo, alisema taarifa waliyopaswa kujibu na Baraza la Wahariri kutokana na ukweli kwamba waliwafikishia taarifa ya kutofika.

Kamuhanda alisema wakati walipopata mwaliko kipindi hicho Wizara ilikuwa katika maandalizi kuhusu kamati za Bunge jambo ambalo liliwafanya washindwe kuhuria kikao hicho ambapo walifikisha taarifa kwa Watendaji wa jukwaaa.

"Kwa kweli nilishangaa niliposoma hiyo taarifa kwa kuwa tulikwisha zungumza kuhusu kutohudhuria kwetu katika kikao hicho.

---
Richard Mwaikenda,
Richard-Mwaikenda.blogspot.com

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts