Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » BAADA YA ASLEY FELLA AMTOA MWANADADA

BAADA YA ASLEY FELLA AMTOA MWANADADA

Written By mpekuaji on Monday, July 30, 2012 | 8:26:00 PM

Miezi  kadhaa baada ya kumtoa  kumnawirisha  kimuziki 'bwamdogo'  Asley kutoka  mitaa ya Temeke jijini Dar, kampuni kubwa ya muziki wa  kizazi kipya Bongo, inayomiliki jina  la 'Mkubwa na Wanawe' sasa  iko tayari kumtoa mavumbini  na kumvisha ustaa wa muziki nchini binti mdogo  anayeitwa  Asna Juma 'Ching Chilla'.

Akizungumza na  mwandishi  wetu  muda mfupi uliopita  'Big Bos' wa  kampuni hiyo  Said Fella Mkubwa Fella amefunguka kuwa  huu ni mwanzo wa mageuzi aliyopanga kuyafanya ndani ya muziki wa kizazi kipya kwa  kuwatoa nyota wa kike ambao walikuwa ama hawapewi nafasi sana kama ilivyo kwa vijana wa kiume.

"Kwa mara ya kwanza tunamtoa msanii mdogo wa  kike, haya ni matunda ya mipango  iliyopo katika kampuni  yetu, kam ambavyo mnafahamu tumewatoa wengi lakini wote walikuwa ni wasanii wa kiume, safari  hii tumeamua kuweka nguvu kwa wasanii wa kike na tutahakikisha wanapata mafanikio kama ambavyo wanapata wasanii wa kiume, hivyo nawaomba wadau wamsapoti binti huyu ambae tumeanza naye ili  kuweka  chagizo kwa wasichana wengine  kujitokeza  na hatimaye tukapata wanamuziki wengi wa kike wenye mafanikio kam ailivyo huko kwa wenzetu. alisema Fella.
 
hapa chini ni video ya wimbo mpya wa  Ching Chilla  so cheki nayo halafu utasema nayo



Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts