
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemuita ikulu mwanamuziki anayefanya vizuri kwa sasa kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ na kumpa SHAVU NONO.
Kwa mujibu wa Diamond, juzikati ‘RAIS’ alimwita ikulu Magogoni, Dar es Salaam na kumpa shavu la kwenda kufanya shoo kwenye mkutano maalum unaofanyika Washington DC nchini Marekani .
“Yaa, rais aliniita akaniambia kuna shoo natakiwa kwenda kufanya Marekani.
“Kwa mara ya kwanza nitasafiri nje ya nchi na madensa wangu wanne na msemaji mmoja. Sasa hivi hawataki kutembea na kupanda magari wasije wakakosa hiyo safari,” alisema Diamond na kuongeza kuwa baada ya kuumwa, mawazo aliyaweka kwenye mchongo huo hivyo mambo mengine yataendelea ikiwa ni pamoja na kufanya kolabo na mwanamuziki wa kimataifa wa Nigeria, J. Martins.
Post your Comment


