MSANII wa filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ amejikuta kwenye bifu zito na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’ baada ya kudai kuwa, kijana huyo anatumia bangi.
Akiongea na mwandishi wetu , Koleta alisema kuwa kitendo cha Ney kuwachana wasanii wa filamu wa kike kuwa wanajiuza si akili yake bali bangi anayovuta ndiyo inayomtuma kusema hivyo.
“Ney huenda anavuta bangi tena anatumia mbichi bila kula, huwezi kusema wasanii wa kike tunajiuza wakati huna ushaidi juu ya suala hilo, bangi zake zinampeleka pabaya,” alisema Koleta.
Post your Comment


