Akiongea na mwandishi wetu, Juliet alisema ameamua kuingia kwa asilimia mia moja kwenye gemu la uigizaji kwa vile amegundua ndiyo fani inayolipa hasa akizingatia kuwa ana kipaji.
Alisema kwa kuanzia anaandaa filamu yake inayokwenda kwa jina la Sister Juliet aliyomshirikisha Sylvia Shally.
“Nimeamua kujikita katika filamu kwa sasa, mradi wa kusaidia walemavu wa ngozi nitaendelea nao baadaye. Kwa kuanzia nimeandaa filamu yangu ya Sister Juliet nikicheza na Sylvia Shally,” alisema Juliet.
Post your Comment


