Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » MRISHO NGASSA AMALIZANA NA SIMBA - ALIPWA MILLIONI 30, GARI NA MSHAHARA WA MILLIONI 2 KWA MWEZI

MRISHO NGASSA AMALIZANA NA SIMBA - ALIPWA MILLIONI 30, GARI NA MSHAHARA WA MILLIONI 2 KWA MWEZI

Written By mpekuaji on Thursday, August 2, 2012 | 7:57:00 PM

Hatimaye leo mchana sakata la usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa akiichezea klabu ya Azam msimu uliopita, kabla ya jana kuuzwa kwenda klabu ya Simba limemalizika.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Simba, leo mchana walikutana na mchezaji mwenyewe ili kuweza kukubalina juu ya mahitaji yake binafsi, baada ya jana wekundu hao wa msimbazi kumalizana na Azam.

Kwenye mkataba wake mpya na Simba, Ngassa atapewa gari aina ya Verossa, ada ya usajili millioni 30 pamoja na kupewa mshahara wa millioni 2 kwa mwezi kama alivyokuwa akilipwa kwenye klabu aliyotoka ya Azam.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari mkataba ni mwaka mmoja.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts