Waziri Kivuli wa Mambo ya ndani amabye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya
chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Godbles Lema ameshauri
kufungwa kwa vifaa maalum vinavyopima ulevi ndani ya bunge ilikulinda
heshima ya Mhimili huo wa Bunge.
Waziri huyo kivuli pamoja na mambo mengine amepongeza uamuzi wa Rais wa
kumfuta kazi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nje Charles Kitwanga
huku akisema ni dhahiri kiongozi huyo amechafua hadhi ya Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Lema amekiri kitendo cha unywaji wa Pombe kupitiliza kwa kiongozi ni
utovu wa nidhamu jambo ambalo huenda likazidi kushusha hadhi ya bunge
ambalo ni Mahususi kwa kutunga sheria na kuisimamia Serikali.
Haya yanakuja ikiwa ni siku moja tu baada ya taarifa ya Ikulu ya Dar es
Salaam kutangaza kumtimua kazi aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya
nchi baada ya kuingia bungeni na kujibu swali la wizara yake kimakosa
huku akiwa amelewa.
Post your Comment



