Video mpya ya Yamoto Band imeachiwa mitaani mapema wiki hii bila ya mwanadada Ruby kuonekana japo ilitafutwa kiki kuwa Rubby anatoka kimapenzi na Dogo Aslay.
Baada
ya Video mpya ya Yamoto Band kuingia mtaani mapema wiki hii bila ya
mwanadada Rubby kuonekana japo ilitafutwa kiki kuwa Ruby anatoka
kimapenzi na Dogo Aslay na hakuna kitu baada ya bendi kumwaga mchele
kwenye 5 Selekt ya EATV na kusema kuwa Ruby kazidiwa.
Tukaona siyo mbaya kumtembelea Mkubwa Fella TMK na kumkuta
anawanoa vijana wengine wapya wa muziki wa Taarab ambao yeye ameamua
kuwaita Moyo Fleva TAR na tulipomuuliza kuhusu kutokuonekana kwa Ruby
kwenye video ya Suu alikua na haya ya kuongea.
Mkubwa Fella alisema sababu ya Ruby kutotokea katika kideo hicho ni
kutokana na msongo wa mawazo amabao ulipelekea kuchukua takribani wiki
mbili wakiwa wanamsubiri lakini ilishindikana ndio wakaamua kuweka
msanii nwingine kwa niaba yake.
Mkubwa Fella alilisitiza kuwa watu wamuelewe vizuri Ruby kwani yeye
ni kama binadamu mwingine anapatwa na matatizo pia na wasichukulie
kwamba anatatizo lolote na Yamoto Band licha ya kuwa na maneno maneno
mengi juu ya kutoonekana kwake kwenye video hiyo.
Post your Comment



