Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN ameiomba
serikali ya MALAYSIA kujenga ofisi za ubalozi wake hapa nchini ili
kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Makamu
wa Rais ametoa kauli hiyo leo Juni 24, 2016 alipokutana na kufanya
mazungumzo Waziri asiye na Wizara Maalum Dkt SRI IDRIS JALA ambaye
aliongozana na Balozi wa MALAYSIA aliye na makazi yake jijini Nairobi
Kenya, ISMAIL SALAM walipomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar
Salaam.
Makamu
wa Rais amesema ujenzi wa ofisi za ubalozi huo hapa nchini utarahisisha
kwa kiasi kikubwa Watanzania wanaotaka kusafiri kwenda nchini MALAYASIA
kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo za masomo na biashara kuliko
hali ilivyo sasa ambapo ofisi za balozi hizo zipo Nairobi – Nchini
KENYA.
Kwa
upande wake Waziri asiye na Wizara Maalum Dkt SRI IDRIS JALA
amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa nchi yake itaendelea
kuimarisha,kukuza na kuendeleza mahusiano na ushirikiano kati ya
Tanzania na Malaysia hasa uanzishaji wa ubalozi wake hapa nchini.
Hata
hivyo, Waziri huyo amesisitiza umuhimu wa kuanzishwa kwa Makubaliano ya
pamoja ya ushirikiano kati ya Tanzania na Malaysia ambayo yatajikita
katika sekta mbalimbali zikiwemo za elimu, uchukuzi na biashara.
Wakati
huo huo, Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN pia amekutana Makamu wa
Rais wa TIGO – Afrika RACHEL SAMREN ambapo wamezungumzia masuala
mbalimbali ikiwemo namna kampuni hiyo itakavyosadia katika kuwawezesha
wanawake kuondokana na umaskini hapa nchini.
Katika kuhakikisha taifa linaongeza ukusanyaji wa mapato,
Makamu
wa Rais ameuhimiza uongozi wa kampuni ya Simu ya Tigo hapa nchini
kuhakikisha unalipa kodi kwa uwazi ili fedha hizo ziweze kusaidia
serikali katika kuimarisha utoaji wa huduma za kijamii hapa nchini.
Post your Comment




