Baadhi ya wabunge na wananchi wameelezea mategemeo na mitizamo yao
katika bajeti ya serikali inayotarajiwa kusomwa leo bungeni ambapo
wengi wao wamesema bajeti hiyo itawasaidia kama itapungunza gharama za
maisha sambamba na kuwasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma bora za
maendeleo.
Dotto Biteko ni mbunge wa jimbo la Bukombe ambaye anasema ni wazi
kuwa bajeti ya sasa itawaweza kuleta mabadiliko ya moja kwa moja kwa
watu wake kwa sababu sehemu kubwa ya fedha zimetengwa kwa ajili ya
miradi ya maendeleo.
Maelezo hayo yanatofautiana na yale ya Mh Abdadalh Mtolea mbunge wa
Temeke kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF ambapo anasema bajeti hi
haiwezi kuwafikisha wananchi sehemu yoyote kwani inasisitiza uchumi wa
viwanda lakini hakuna hata shilingi moja iliyotengwa kwa ajili ya ujenzi
wa viwanda.
Mh Stepheni Ngonyani ni mbunge wa Korogwe vijijini ambaye anasema
wananchi wanachotaka ni kuona bajeti itakayowasilisihwa inajibu kero
mbalimbali kama kupungua kwa bei za bidhaa mbalimbali kama Sukari,
Misamaha ya kodi sambamba na uboreshwaji wa huduma za kijamii.
Naye waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za serikali za
mitaa Mh George Simbachawene amesema bajeti inayotarajiwa kusomwa
bungeni wananchi wanapaswa kujua kuwa serikali inategemea kodi katika
kuitekeleza na hivyo wahakikishe wanalipa kodi kwa wingi ili bajeti
ziweze kutekelezeka kiurahisi.
Post your Comment



