Mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasi na Maendeleo
(CHADEMA), Joseph Mbilinyi amesimamishwa kuhudhuria na vikao 10 vya
Bunge kuanzi leo kufuatia kitendo cha kuonyesha kidole cha kati bungeni.
Joseph Mbilinyi alitenda kosa hilo alipokuwa akitoka nje ya ukumbi wa
Bunge baada ya kile alichoeleza kuwa kuna mbunge wa CCM aliyemtusi mama
yake. Hata hivyo alipohojiwa kama anamfahamu mbunge huyo, Mbilinyi
alisema kuwa hamfahamu.
Hukumu hiyo imesomwa leo na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson
baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Bunge kueleza kuwa kamati
hiyo ilijiridhisha kuwa kitendo kilichofanywa na mbunge huyo kuwa ni
kosa.
Aidha wabunge wangine waliosimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge ni
pamoja na Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo, James Ole Millya Mbunge wa
Simanjiro kwa makosa yanayofanana ya kusema uongo bungeni. Wabunge hawa
wamesimamishwa kuhudhuria vikao vitano kuanzi leo.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameahirisha
mkutano wa tatu wa Bunge lililokuwa na lengo la kujadili na kupitisha
bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2016 2017. Kufuatia kuahirishwa
huko, kuanzia kesho Julai Mosi, serikali itaanza kutekeleza miradi na
mpango mingine iliyoanishwa katika bajeti hiyo.
Post your Comment



