Msanii Roma Mkatoliki ambaye ameachia ngoma yake mpya 'Kaa tayari'
amefunguka na kusema moja ya mstari uliopo kwenye wimbo wake huo
unamuhusu meneja wa Diamond Platnumz ambapo unamchana kuwa saizi
anamganda sana Diamond Platnumz mpaka amelisahau kundi lake na Tip Top Connection.
Roma Mkatoliki amedai kabla ya wimbo huo haujatoka aliweza
kusimkilizisha Babu Tale kisha Bab Tale alimchimba mkwara kuwa usipofuta
huo mstari wimbo wako hautatoka, Roma aliongea huku akiwa anacheka
kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio.
Kwa upande wake Babu Tale aliibuka kwenye kipindi hicho na kuja
kujibu tuhuma hizo na kusema yeye hajalisahau kundi hilo kama ambavyo
Roma Mkatoliki alivyoimba bali anadai wao wana mipango, ndiyo maana
alianza kuja Madee na Miguru pande, akaja Dogo Janja na 'My Life' na
baadaye atakuja Tunda Man, hivyo hajalisahau kundi hilo kama alivyosema
Roma Mkatoliki kwenye wimbo wake huo.
"Unajua saizi Babu Tale ni meneja mkubwa Afrika, nimemzidi Roma
Mkatoliki kwa kila kitu, nimemzidi followers, busara, hadi dhambi
nimemzidi, hivyo Roma Mkatolik mimi nadhani ameimba huo mstari kwa kuwa
anajua mimi ni mtu mkubwa hivyo alikuwa anataka wimbo wake uweze kufanya
vizuri ndiyo maana akanichana mle, japo alichoimba hakina ukweli"
alisema Babu Tale.
Kwa upande wa Said Fella alisimama upande wa Roma Mkatoliki na kudai
alichoimba Roma Mkatoliki ni maneno ambayo hata mtaani yapo kwani watu
wamekuwa wakisema kuwa viongozi hao saizi wameyasahau makundi yao ya
zamani.
"Unajua Roma ni mtu mzima, alichoimba hata mtaani huko watu wanasema,
na unaweza kuona labda Roma ameambiwa hayo maneno na msanii kama Madee
au msanii mwingine yeyote wa kwetu, lakini hata mimi nilishawahi
kumwambia mdogo wangu Babu Tale kuwa tufanye yote lakini yeye asiisahau
Tip Top Connection na mimi nisiisahau TMK" alisema Said Fella.
Post your Comment



