KING wa R&B Bongo, Bernad
Paul ‘Ben Pol’ anatarajiwa kuja na remix ya ngoma yake mpya ya Moyo
Mashine akiwa amemshirikisha staa wa kimataifa (jina kapuni).
Akipiga stori mbili-tatu na mtandao wetu, Ben
Pol aliyewahi kubamba na Ngoma ya Sophia na Samboira alisema kuwa,
mbali na remix hiyo pia atafanya ziara (Moyo Mashine Tour) nchi nzima.
“Ujue kwanza Moyo Mashine maana yake ni
moyo kushindwa kuleta majibu ya upendo wakati kazi yake ni kuleta
upendo. Nafurahi ngoma kupokelewa vizuri lakini niwaambie remix yake
itakuwa mara mbili ya hii kwani nitatoka na staa wa kimataifa,” alisema
Ben Pol.
Post your Comment


