Wasanii wengi kwa sasa wanashindana na soko la muziki ili kuhakikisha
wanapenya kimataifa na kuweza kuutangaza vyema muziki wa tanzania na
ndio sababu ya kupanda ndege kwenda kutafuta mandhari pamoja na video
kali.
Mfalme wa sauti bongo kama anavyojiita Christian Bella
ameweka wazi suala lake la kwenda nchini Afrika Kusini kufanyia video
wimbo wake mpya utakao kwenda kwa jina la Nishike huku msanii wa
mashairi ya hip hop Fid Q akiwa muandaaji wa script.
"nimekaa
muda mrefu bila kuachia wimbo, sasa nitaenda na bw. Farid kwa ajili ya
kunichorea script kwani tulipokua sweeden nilimuona akichora script na
nikagundua ni muandaaji mzuri”.
Bella amesema pia bado kuna wimbo
ambao ameshirikiana na Fid Q na yeye ameimba kiitikio hivyo mashabiki
wautarajie wimbo huo kwani upo karibuni kuachiliwa.
Post your Comment