Harmonize amefafanua kuwa chumba kinachoonekana kwenye video ya
‘Matatizo’ ndicho chumba chake alichokuwa anakaa huko Kiwalani kabla
hajawa staa.
Akiongea nasi, Harmonize alisema kuwa kuimba
nyimbo za matatizo uliyowahi kupitia zinasaidia kuwa inspire watu japo
wengine wanadai kuwa kufanya hivyo ni ushamba.
“Muda mwingine kueleza matatizo uliyoyapitia ni kama ushamba hivi,
muda mwingine kueleza vitu ulivyopitia ni kitu kizuri kwa kuwa unawa
inspire vijana wengi sana ambao wapo mtaani hata wazee pia waliokaribia
kukata tamaa,” alisema Harmonize.
“Kwenye video ya matatizo kwa asilimia kubwa vyote nilivyoimba ni
historia yangu kabisa. Hata kile chumba nilichoshoot video ndio chumba
nilichokuwa nimepanga wakati nakaa Kiwalani,” aliongeza.
Aidha Harmonize aliongeza kuwa wakati anakaa kwenye chumba hicho aliweka kapeti lake la bei rahisi na kigodoro pekee.
Post your Comment



