Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli hivi karibuni katika ziara zake alikutana na kijana aliyemshangilia kwa nguvu zake zote hali ambayo ilimfanya mkuu huyo wa nchi kumwita na kupiga naye picha.
Kijana huyo ambaye anaitwa Omar Abdalah Ramadhani ‘Mkereketwa wa
Mwendokasi’ alisikika akisema “Magufili kule aliko, aminia mzazi, Mungu
akupe baraka zote mzazi, na asiyekupenda Mungu atamtokomeza, Watanzania
tuko nyuma yako” kauli iliyomfanya Rais Magufuli amwite ili apige naye
picha na baadaye kuombewa dua na kijana huyo.
Baada ya tukio hilo kufanyika na kurekodiwa, kijana huyo anaendelea
kuwa maarufu katika mitandao ya kijamii huku baadhi ya watu wakiwa
amepachikwa jina la ‘Shabiki wa Mwendokasi’.
Post your Comment



