Waziri
wa Katiba na Sheria nchini Dkt. Harrison Mwakyembe amesema Serikali
kupitia mamlaka ya wakala wa usajili, ufilisi na udhamini (RITA)
inatarajia kuzifutia usajili bodi 500 za udhamiri kutokana na bodi hizo
kuacha kufanya kazi zake kiufanisi na kuisababishia serikali hasara ya
fedha ambazo zinatumika bila kuwa na faida kwa Watanzania.
Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati
akizungumza na bodi ya Mamlaka ya Rita kwa lengo lakufanya marekebisho
mbalimbali sambamba na kuweka sheria maalumu ambayo itaipa uwezo bodi
hiyo yakuzifutia usajili bodi zote ambazo zinafanya kazi chini ya
kiwango.
Amesema Serikali imedhamiria kuongeza na kudhibiti mapato ya nchi
sambamba na kuhakikisha bodi zote zilizosajiliwa na ambazo zinapata
ruzuku ya Serikali zifanye kazi yake kama ilivyokusudiwa hasa zile za
dini na za kijamii.
angalia video hii hapa chini
angalia video hii hapa chini
Post your Comment


