Watu tisa wanakishikiliwa na
jeshi la polisi mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kukutwa wakifanya biashara ya
dawa za kulevya aina ya bangi kilo 96 na kete 176 huku wengine wawili
wakikamatwa na pombe haramu ya gongo lita 67.
Akizungumza Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Zuberi Mwombeji (pichani) aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni Gabriel Ndabaliuze (37), mkazi wa Bombambili,
Evance Mkonde (24), mkazi wa Lizaboni na Gwaita Shaib (35), mkazi wa
Namanditi ambao kwa pamoja walikamatwa na bangi kilo 34 maeneo ya
Matarawe, Songea Mjini.
Kamanda Mwombeji alisema kuwa watuhumiwa
wengine, Costa Mwinuka (49), mkazi wa Mkuzo, Angeleus Hyera (39), mkazi
wa Lupapila na Zamtanga Gama (42), mkazi wa Mjimwema walikutwa eneo la
Sido, Songea wakiwa na bangi kilo 41.
Aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni
Felician Mgaya (44), Mustapha Rashid na Mrisho Mponda (19), wakazi wa
Hoahoa Mbinga, ambao walikamatwa na bangi kilo 7 na kete 132 na Hija
Omari Hashimu, mkazi wa Nakapanya, Tunduru aliyekamatwa na bangi kilo 5.
Kamanda huyo aliongeza kuwa watuhumiwa
wengine, Hassan Mtulule (32) na Twalib Abbas (30) wakazi wa Tunduru
walikamatwa na pombe haramu ya gongo lita 67 na kwamba upelelezi
unaendelea na mara utakapokamilika, watafikishwa mahakamani kujibu
tuhuma zinazowakabili.
Post your Comment


