Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Leonard Lutegama Maboko
kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS).
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 07 Julai, 2016.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Leonard
Lutegama Maboko alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa
Magonjwa ya binadamu Mbeya (NIMR Mbeya).
Dkt. Leonard Lutegama Maboko anachukua
nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Fatma Mrisho ambaye mkataba wake
umemalizika tangu tarehe 30 Juni, 2016.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
08 Julai, 2016
Post your Comment


