KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida
kijana mwenye tatizo la ulemavu wa viungo na akili, amegundulika
kufungiwa ndani kwa zaidi ya miaka 11 na wazazi wake katika eneo la
Mwambenja Kata ya Ilemi Jijini hapa.
Kijana huyo, mwenye umri wa miaka 20, ambaye amejulikana kwa jina la
Fredrick Emmanuel ametajwa kuwa amekuwa akiishi ndani bila ya kutolewa
nje hali iliyochangia kwa kiasi kikubwa kudhohofisha mwili wake .
Mmoja wa majirani ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa
Kijana huyo licha ya kuzaliwa akiwa na ulemavu wa viungo vya mikono na
miguu, pia amezaliwa akiwa na utindio wa ubongo hali inayomfanya
kushindwa kuongea.
Amesema wazazi wa mtoto huyo wamekuwa wakimfungia ndani ambapo hata
wao hawakuluhusiwa kuingia ndani ya nyumba hali iliyowafanya washituke
na kutoa taarifa ili kumuokoa kijana huyo.
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa mtaa wa Mwambenja, Rosemary
Jama, amesema taarifa za Ferdrick kuishi ndani ya nyumba hiyo walikuwa
nazo lakini hawakuwahi kupata taarifa za kwamba kijana huyo hatolewi
nje.
“Sisi tunafahamu ndani ya nyumba ya Emmanuel kuna mtoto ambaye ni
mlemavu lakini hatukuweza kufahamu mazingira anayoishi kijana huyu,
nimeshuhudia kweli huu ni unyanyasaji wa kijinsia, licha ya kutotolewa
nje lakini kijana huyu anaonekana amekosa chakula,”alisema.
Akizungumza huku akionesha kutojali, Baba wa kijana huyo Emmanuel
John, anasema mwanae Fedrick, alizaliwa mwaka 1996 ukiwa ni uzao wake wa
kwanza katika familia hiyo na akufuatiwa na wenzake watatu ambao wote
mungu amewajalia na kuzaliwa wakiwa wazima.
Kufuatia tukio hilo baadhi ya majirani wameomba mamlaka husika
kuingila kati ili kumsaidia kijana huyo kwani maisha yake yapo hatarini
kutokana na wazazi kutoonesha kujali.
Post your Comment



