Waswahili husema: “lisemwalo lipo kama halipo laja’. Usemi huu umedhihirika baada ya kuwepo tuhuma siku nyingi kuwa rapa David Genzi maarufu Young D kuwa anatumia dawa za kulevya naye kuzikanusha kila mara.
Hatimaye Young D ameamua kuutua mzigo huo na kukiri
kuwa kwa zaidi ya mwaka mmoja amekuwa akitumia dawa za kulevya pamoja na
kukiri kilichomwingiza huko.
Kama ulifikiria rapa Young Dee
alitumbukia kwa bahati mbaya katika matumizi ya dawa za kulevya,
mwenyewe ameiambia Starehe kuwa alifahamu fika kwamba anaingia kwenye
unga tofauti na wengine wanapoanza kutumia kwa mara ya kwanza.
Wasanii
wengi waliokiri kutumia dawa za kulevya wamekuwa wakitoa ushuhuda kuwa
walianza bila kujua. Wengi hueleza kuwa walianza kwa kuwekewa katika
bangi au sigara na marafiki, wapenzi au wafanyabiashara.
Young Dee
ameyasema hayo wiki moja baada ya kutangaza rasmi mbele ya vyombo vya
habari kuwa amekuwa akitumia unga kwa kipindi cha mwaka mmoja kabla ya
kuamua kuacha na kupatiwa matibabu na wanasaikolojia.
Akizungumza
mapema wiki iliyopita alisema kitu kilichomvuta kutumia dawa za kulevya ni
kundi la marafiki ambalo alikuwa akiambatana nalo kipindi alipolegalega
katika kazi zake za muziki.
Post your Comment



