Mkurugenzi wa label ya ‘MDB’ ambayo inamsimia rapper huyo, Max Rioba, kupitia instagram yake ameandika haya kuhusu rapper huyo.
“Namwomba Maulana akusimamie mwanangu uendelee kufanya vizuri na
uishangaze dunia na walimwengu wakaao ndani yake. Shikilia hapo hapo
uliposhikilia, utafanikiwa tu,” alisema Max.
“Muamini
Mungu, muombe yeye akupe ujasiri wa kuushinda moyo kila unapohisi
unakaribia kuanguka. Akupe akili za utambuzi uone kisiki kilichoko mbele
yako kabla hujajikwaa. Awabariki wale wote wanaochukia maamuzi yako na
kuwabariki zaidi wanaokuunga mkono, nayaandika haya kutoka moyoni mwangu
Dee. Naamini una nyota inayoweza kung’aa hadi mbali sana,”
Aliongeza, “Najua
wako watu wengi sana wanaochukia sana hii movement, Lakini kamwe
usiwasikilize. Uliamua mwenyewe kuanguka, ukaamua mwenyewe kuamka. Amua
mwenyewe kushikilia msimamo wa mabadiliko yako. Kuna kijana mwingine
anaepitia mambo kama uliyoyapitia anasubiri aone umesimama imara naye
apate nguvu za kunyanyuka. Fight for yourself, work it out, force your
damn self to stay up tight, to stay on top. Then uone utakavyofanikiwa.
You’re not a star Dee, you’re a megastar, bigger than a superstar!!!
Hands Up y’all. I’m done,”..
Post your Comment


