Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Injinia James Fransis Mbatia amesema kwamba
maamuzi yoyote ambayo kambi ya upinzani itayafanya endapo wataitwa na
kamati ya maridhiano juu ya kususia Bunge wao watakachoangalia ni
maslahi ya kitaifa.
Injinia
Mbatia ameyasema hayo kuhusu hoja ya wao kukutanishwa na
kamati ya maridhiano kujadili kitendo chao cha kususia bunge la bajeti.
''Sisi kabla ya kufanya jambo lolote tunaangalia mama Tanzania
kwanza, swala la maridhiano limekuwa jambo letu mara zote , tangu
tumeanza masuala ya katiba pamoja na mambo ya demokrasia tuna'' amesema
Mbatia.
''Sisi hatujadili mtu tunajadili mfumo, Bunge kwa mujibu wa katiba
linatakiwa lisimamie serikali na kuishauri kwa kuheshimu utu na
kuhakikisha yale tunayoyafanya yanakuwa na maslahi ya taifa'', Amesema
Mbatia.
Mgogoro wetu na Naibu Spika ni kwamba anaongoza Bunge kwa kuagizwa na
serikali na hii itaonekana wazi kwamba hoja ya maslahi ya wabunge
wabunge wa CCM waliosema hapana walikuwa ni wengi na walikuwa wao kwa
wao lakini akasema anatumia kura ya veto hivyo hoja hiyo imepita.
Mbatia amehitimisha kwa kusema watanzania wategemee kama hali ya
maridhiano haitapatikana wategemee mambo hayohayo ya kususia mambo
kurudi kwenye jamii mfano tuu suala la VAT, serikali imeshindwa
kulifafanua kwa kuwa waziri amesema la kwake, gavana wa benki akasema la
kwake, na mkurugenzi wa TRA akasema la kwake.
Post your Comment


