Baadhi ya wasanii wa filamu Bongo waliowahi kufanya uamuzi wa
kubadili dini kutoka kwenye Ukristo kuingia kwenye Uislam
‘wametumbuliwa’ kufuatia mienendo yao isiyokubalika.
Masupastaa hao wakiwemo Jacqueline Wolper, Rose Ndauka, Flora Mvungi,
Aunt Ezekiel na Ester Kiama wametumbuliwa kutokana na kutoonesha
jitihada zozote za kuijua vilivyo dini waliyoiendea.Akizungumza na Ijumaa, hivi karibuni, Shehe Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum alisema kuwa, kitendo cha mtu
kubadili dini kisha kutoonesha utofauti hakuna maana na ni bora kubaki
kwenye dini ya awali
“Kwanza wanaokosea ni wale wanaowasilimisha maana wakishawabadili dini
hawafanyi jitihada za kuwatafutia watu wa kuwafundisha misingi ya Dini
ya Kiislam, matokeo yake sasa unakuta mtu amebadili dini na kupewa jina
la Kiislam lakini hafuati misingi ya dini.
“Lakini pili, hawa wanaobadili dini
wenyewe hawaoneshi kutaka kujifunza, wanaridhika na ile hali ya kuambiwa
wamesilimu na kupewa majina mazuri ya Kiislam lakini baada ya hapo
wanabaki walewale,” alisema shehe huyo.
Wolper, Rose, Flora, Aunt na Ester ni
kati ya wasanii wa Bongo waliosilimu huku baadhi yao wakifanya hivyo
kufuata imani za wachumba zao ili waolewe lakini mpaka sasa hakuna
aliyeonesha utimilifu wa kusilimu kwake, badala yake baadhi yao
wameendelea na mifumo yao ya maisha kama walivyokuwa wakiishi walipokuwa
Wakristo.
Post your Comment





