Justine Ambrose (30) ambaye ni
mtoto wa kigogo mmoja wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, ametiwa
mbaroni kwa tuhuma za kumbaka denti wa kidato cha kwanza Shule ya
Sekondari Kigonseram tukio lililotokea Julai 2, mwaka huu.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo,
kamanda wa polisi mkoani hapa, Zubery Mwombeji alisema lilitokea usiku
katika Kijiji cha Kitai muda mfupi baada ya mwanafunzi huyo mwenye umri
wa miaka 14, kushuka kutoka katika gari lililomtoa kijijini kwao
Ngingama, Lituhi akielekea shuleni kwao.
Alisema aliposhuka, mtuhumiwa huyo
ambaye pia ni mfanyakazi wa kukusanya ushuru wa Halmashauri ya Mbinga
katika geti la Kitai, alimshika kwa nguvu na kumwingiza kwenye kibanda
cha walinzi, ambako licha ya kupiga kelele zilizokosa msaada, alimfanyia
unyama huo na kumwachia maumivu makali.
Katika wodi maalum ya wagonjwa
wanaotibiwa kwa bima ya afya, mwandishi wetu alimshuhudia mtoto huyo
akiwa na hali mbaya, huku akizungumza kwa shida.
“Wakati anatumia nguvu ya kunivuta
kuelekea kwenye kile kibanda nilikuwa nikipiga kelele, yeye alikuwa
akikazana kuniziba mdomo lakini sikupata msaada wowote mpaka
alipofanikisha kitendo chake cha kunifanyia unyama huu,” alisema mtoto
huyo alipotakiwa kufunguka kuhusu kilichomsibu.
Alisema kutokana na maumivu makali
aliyokuwa nayo baada ya kitendo hicho, alishindwa kwenda popote na
kulazimika kulala ndani ya kibanda hicho hadi kesho yake ambapo
wasamaria wema walimpa msaada wa kumsa risha Kituo cha Polisi cha Wilaya
ya Mbinga ambako alipatiwa hati namba tatu ya polisi (PF 3) na kwenda
kutibiwa.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya
Mbinga, Elisha Robert alithibitisha juu ya kubakwa kwa denti huyo,
lakini alikataa kutoa maelezo zaidi.
Post your Comment


