Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » Afande Sele Atiwa Mbaroni

Afande Sele Atiwa Mbaroni

Written By Vuvuzela on Thursday, September 1, 2016 | 9:00:00 AM

Msanii mkongwe wa muziki kutoka Morogoro, Afande Sele amedai anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro kwa madai anagawa pesa kwa watu ili kuwashawishi wajitokeze katika maandamano ya UKUTA ambayo yamepigwa marufuku.
Rapper huyo ambaye ni mwanasiasa na aligombea ubunge kupitia cha ACT Wazalendo katika uchaguzi uliyopita, amedai yupo mikononi mwa polisi toka jana.

“Huku ni kushindwa kama sio kufeli, toka jana nipo mikononi mwa polisi eti naambiwa nimeratibu mkutano wa UKUTA , nimechapisha T-shirt na kugawa fedha ili kesho watu waandamane, pia kuaandaa mkutano maeneo ya Msamvu.,” aliandika Afande Sele kupitia facebook yake.

Aliongeza, “Nina zaidi ya mwezi sijakaa maeneo ya Msamvu zaidi ya kupita nikiwa naelekea mikoani tena nikiwa kwenye gari yangu. Ila hii aibu na fedheha kwa jeshi la polisi, maamuzi ya kukurupuka . Tusubiri,”

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts