Mara nyingi mtu wako wa karibu anapokuwa anasherehekea siku yake ya
kuzaliwa, ni muhimu kumpa ujumbe muhimu kuonesha jinsi alivyo na maana
kwako.
Vanessa Mdee ametumia siku ya kuzaliwa ya mpenzi wake, Jux
kumwandikia ujumbe muhimu kudhihirisha ni kwa kiasi gani anampenda.
Ametumia pia fursa hiyo kuutaja wimbo wao wa pamoja, Juu. Usome:
"When we first met I was an upcoming songstress with a
fast tongue and one hit song on the radio. You … well you were pretty
much the same. Your boy asked me if I would spit some bars on your song.
I said no. Then walked into the studio and met you and instantly had a
change of heart. Fast forward to 2yrs later, tumekuwa.
You’ve got the biggest song in the country #Wivu and a multi million
dollar brand #AfricanBoy and as for me well … kitu kimoja hakijabadilika
though. Kwako sisikii. Lol!
Lakini hayo yoteee ni mifano tu ya jinsi gani ukiwa na mahusiano na
mtu anayekujenga kifikra na vinginevyo maisha yako yanaweza kukaa sawa.
Siwezi kueleza ni jinsi gani uwepo wako katika maisha yangu
yamenibadilisha na kunikuza na kuniboresha. All things are God’s design.
Namuomba Mungu akuongoze and akupe maisha marefu sana sana sana. Maisha
yenye mafanikio, afya bora na furaha tele. Una moyo wa kipekee sana
tofauti na mtu yeyote ninayemfaham.
Nasikitika kuwa mbali na wewe leo hii lakini unajua nikipata, umepata
na tunazidi kwenda #Juu. Oh by the way kwa mashabiki wetu ngoma yetu ya
kwanza ya pamoja inaitwa
#Juu Basi nisaidieni kumtakia mpenzi wangu Heri ya siku ya kuzaliwa."
#Juu Basi nisaidieni kumtakia mpenzi wangu Heri ya siku ya kuzaliwa."
Post your Comment



