Msanii wa bongo fleva Juma Jux anayetamba kwa sasa na ngoma yake ya
‘Wivu’ amesema kabla hajafanikiwa kimuziki alikuwa akitumia vitu vya
nyumbani kwao kusumbua na kuuzia sura mjini.
Jux ameweka wazi kuwa hapo mwanzo alikuwa akitamba mjini kwa mali za
wazazi wake ila kwa sasa hawezi kufanya tena hivyo bali anapambana kiume
kwa kulipa kodi na kujiwekeza kimaisha.
Akiongea na eNewz, Jux amesema “Kwa sasa nina duka nalipa kodi ya
nyumba nina gari naliangalia na pia nimepanga nyumba nalipa kodi, mwanzo
nilikuwa nasaidiwa na wazazi wangu hapo nyuma na kila mtu anapenda
kusaidiwa”
Hata hivyo mbali na kupitia maisha ya kutegemea vya ‘bwerere’ toka
kwa wazazi, Jux hajaona kama ilikuwa tatizo bali ameshauri wazazi
wengine waweze kuwasaidia watoto wao ili waweze kufikia malengo yao kwa
kila namna.
Post your Comment



