Katika kuadhimisha kifo cha mama yake mzazi aliyefariki August 1 miaka
kadhaa iliyopita, Shaa atafanya show mkoani Mtwara, katika sikukuu ya
Eid El Haji, Jumatatu Septemba 12.
Alisema kuwa show hiyo pia itakuwa maalum kwa mashabiki wake
wa mikoa ya Kusini ambako mama yake anatokea. Pia amesema kuwa kwenye
show hiyo itakayofanyika Makonde Beach Club, atatumbuiza pamoja na live
band.
Shaa amedai kuwa show hiyo ilitakuwa ifanyike katika wiki ya
kuadhiminisha kifo cha mama yake lakini aliombwa aisogeze hadi siku ya
Sikukuu.
“Bado ni siku siku nzuri naona ilmradi nitaweza kuonana ana kwa ana na mashabiki wangu huko,” amesema Shaa.
Show hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano na kituo cha Radio cha Pride FM ya Mtwara pamoja na Kings Entertainment.
Post your Comment



