Malkia wa filamu Wema Sepetu amekunwa na wimbo mpya wa
Diamond Platnumz ‘Salome’ na kuamua kujirekodi video huku akiimba wimbo
huo.
Diamond alipost video instagram inayomwonyesha mwigizaji huyo akiimba
wimbo ‘Salome’ huku akiandika ujumbe wa kuonyesha kufurahishwa na
kitendo hicho.
“Hivi huku patakuwa ni kupatwa kwa nini?. Tisha sana ‘Salome’ wake
Idris Sultan full Video link in my BIO and @rayvanny Bio,” aliandika
Diamond kupitia instagram.
Hatua hiyo huwenda ikafungua njia zaidi kwa wawili hao kuaidia katika mambo yao.
Post your Comment



