WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Akaingia kwenye moja ya chumba na mimi nikaingia pasipo kubisha hodi, gafla macho yangu yakakutana na Regina akiwa mtupu kama alivyo zaliwa huku mwili wake ukiwa umejaa maji, akionekana kutoka kuoga, nikatazama kila kona ya chumba na sikumuona binti ambaye nilikuwa ninamfatilia, Regina hakuonekana kushangaa wala hukuficha sehemu zake za siri, zaidi akabaki akiwa ametabamu na kuanza kupiga hatua za kunifwata, gafla nikastukia mlango ukifunguliwa nyuma yangu na nilipo geuka nikakutana na Rahma akiwa anatushangaa
ENDELEA
*Eddy ndio unafanya nini hapo?”
Rahma alizungumza huku akinitazama kwa hasira,
“Kwani wifi wewe, unatuona tunafanya nini?”
Regna alimuuliza swali Rahma, ambalo likazidi kumkasirisha Rahma
“Koma wewe, sijazungumza na wewe, nimemuuliza mume wangu”
“Ndio unijibu sasa, umetukuta tumesimama unababaika, ungenikuta nimemuweka kifuani mwangu si ndio ungekufa”
Regna alizungumza kwa dharau wala sikujua ujasiri kama huu ameutolea wapi, Rahma akanipiga kikumbo, nikastukia akimvaa Regna na kumuangusha chini, na kuanza kupigana, nikabaki nikiwa ninashangaa, sikujua hata nifanye kitu gani, Regna akamgeuza Rahma na kumkalia tumboni mwake, na kuanza kumtandika vibao vya mashavu, Rahma naye hakubaki nyuma, akajikakamua hadi akafanikiwa kumuweka Regna chini ambaye yupo uchi, na kuanza kunzaba makofi ya hasira.Nikamkimbilia Rahma na kumuwahi mikono yake, na kumchomoa mikononi mwa Regna
“Rahma, tulia mke wangu, mbona unataka kuleta aibu kwa wageni waliofika hapa”
Nilizungumza huku nikiendelea kumshikilia Rahma kwa nguvu
“Niache nimkomeshe huyo malaya wako”
Rahma alizungumza huku akijikakamua kutoka mikononi mwangu
“Malaya mwenyewe, hivi unadhani utaweza kuwa peke yako, na ninakuambia ni lazima nimchukue huyo mume wako, kwanza mwanamke mwenyewe huna kizazi, unadhani mume wako ataendelea kukaa na mwanamke tasa kama wewe? Uyooooo”
Maneno ya Regna yalizidi kunishangaza kwa maana si kawaida ya mtu anaye jitambua kuzungumza mambo kama hayo
“Eddy niachie, nimfundishe adabu huyu malaya, hawezi kunvunjia adabu ndani ya nyumba yangu”
“Rahma tulia, ninakuomba utulie mke wangu”
“Unamtetea huyo malaya wako eheee, niache sasa”
Nikastukia Rahma akinipiga kisukusuku cha tumbo na kujikuta nikimuachia, akamvamia Regna na kumuangusha chini, kwa haraka nikafunga mlango, kuepuka watu wa nje kusikia kitu kinacho endelea ndani ya chumba.Rahma akazishika nywele nyingi za Regna na kuanza kukibamiza kichwe chake kwenye kwenye sakavu yetu ya kisasa, Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio baada ya kumuona damu zikiwa zinasambaa chini, zikitoea kwenye kichwa cha Regna.Kwa haraka nikavuta Rahma kwa nguvu zangu zote na kumzuia kuendelea kumpigiza Regna kichwa chake chini
“Achaa,”
Nilizungumza huku nikimbeba juu juu Rahma na kukandamiza ukutani, tangu nianze kumjua Rahma sikuwahi kumuona akiwa na hasira kiasi hichi, Nikaendelea kumkandamiza Rahma ukutani, tukiwa tunatazama kwa macho makali, kidogo hasira yake ikaanza kumtulia.Nikageuka nyuma na kumtazama Regna nikakuta akiwa ametulia kimya huku damu zikiendelea kusambaa kwenye sakafu, nikamfwata kwa haraka sehemu aliyo lala na kukiweka kiganja vhangu kifuani mwake na kukuta mapigo yake ya moyo yakiwa yametulia kimya, nikazidi kuchanganyikiwa
“Ameshakufa”
Nilizungumza huku nikimtazama Rahma ambaye mwili wake wote unamtetemeka kwa woga
“Rahma umeua”
Niliendelea kuzungumza huku nikimpima mapigo ya moyo Regna ila hapakuwa na msukumo wowote, wa mapigo ya moyo ulio endelea kwenye kwenye kifua chake, Nikasikia mlango ukigonjwa kwa nje ikiashiria kuna mtu anahitaji kuingia ndani ya chumba hichi
Tukatazamana na Rahma, na hakuna aliye yanyua kinywa chake kusikilizia hodi inayo gongwa, mtu anaye enedelea kugonga mlango kama dakika tatu hivi kisha akaanza kuita jina
“Regna mke wangu fungua mlango, kuvaa gani masaa kumi”
Ilikuwa ni sauti ya kiume ambayo, ilizidi kuniogopesha, nikapeleka macho yangu kwenye mkono wa kushoto wa Regna na kukuta akiwa amevaa pete ya ndoa akiashiria ni mke halali na huyo anaye gonga mlango
“Wewe mwanamke mimi naondoka zangu, saa utakodi bajaji, nakwenda zangu home kulala muda umesha kwenda”
Jamaa alizungumza na kuzidi kutuchanganya akilia mimi na Rahma, Rahma akataka kuzungumza ila nikawahi kukiweka kidole changu kimoja mdomoni mwangu nikimuashiria kukaa kimya na asizungumze jambo la aina yoyoye.Nikasimama na kwenda kusimama mlangoni na kuliweka sikio langu kwenye mlango na kusikilizia kama jamaa atakua ameondoka.Nikastushwa na mlango kugongwa, tena kwa nguvu
“Wewe mama Junio, hunisikii humo ndani, au mimi ninaondoka”
Nikameza fumba jingi la mate na kubaki nikimtazama Rahma, ambaye sura yake yote imejaa machozi mengi, akijilaumu kwa kitu alicho kifanya.Nikasikia miguu ya mtu akija, na kusimama kwenye mlango
“Afande Denis mbona hapa?”
“Ahaaa si huyu wifi yeko ameingia humu kutoka, hatoke aliniambia kwamba amekuja kubadilisha nguo”
“Alaa labda ameshatoka, na kama nimepishana naye kule kwenye bustani anakutafuta wewe”
“Ahaaa, atakuwa ametoka saa ngapi?”
“Mpigie simu?”
“Simu yake imezima chaji na ninayo mimi”
“Hembu kamcheki kwenye bustani kule”
“Sawa”
Nikasikia miguu ya watu hao ikiondoka nje ya malango jambo lililo anza kunichanganya na kuhisi kwamba kuna mauza uza yanaendelea kwenye hii nyumba yangu
“Ngoja nakwenda nje mara moja, kaa humu ndani na ufunge mlango kwa nje sawa”
“Unakwenda wapi mume wangu?”
Rahma alizungumza huku akinyanyuka, kutoka sehemu alipokuwa amekaa
“Nimekuambia kaa humu ndani kuna kiitu ninakwenda kukitazama nje sawa”
“Unaniacha peke yangu, humu ndani na hii maiti?”
“Nimekuambia, kaa humu sawa”
Ilinibidi nizungumze kwa ukali kidogo na kumfanya Rahma kustuka na kubaki akiwa amesimama
“Funga mlango kwa ndani na usimfungulie mtu wa aina yoyota zaidi yangu sawa”
Rahma alinijibu huku akitingisha kichwa akionekana kunielewa na kukubaliana na mimi kishingo upande.Nikafungua mlango taratibu na kuchungulia kwenye kordo, sikuona mtu yoyote
“Funga sasa”
Nikatoka haraka, na kumuacha Rahma akifunga kwa ndani, nikapiga hatua za haraka kuelekea nje kwenye bustani, nikasimama sehemu ambayo nitaweza kuwaona watu wote waliopo kwenye bustani, ila sikumuona Regna wala mume wake
“Kaka Eddy unatafuta nini?”
Jamaa mmoja aliniuliza baada ya kuniona nikiwa ninapepesa macho yangu kila kona ya bustani yangu
“Kuna dada, hivi ni muandishi wa habari sijui unemuona?”
“Yupoje yupoje”
“Mrefu, kiasi na mwembamba fulani?”
“Huyo atakuwa ni Regna?”
“Eheee huyo huyo”
“Nimemuona akielekea kwenye parking za magari”
“Asante”
Nikaachana na jamaa na kuanza kupiga hatua za kwenda kwenye maegesho ya magari, nikakutana na gari moja aina ya Vitz, ikasimama pembeni yangu na kioo cha gari hilo kikashushwa
“Kaka Eddy, nilikuwa ninakutafuta nikuage”
Sauti ya jamaa ndio sauti ya jamaa aliyekuwa akigonga mlangoni, akimuita mke wake, nikabaki nikishangaa baada ya mlango wa upende wa pili wa dereva ukifunguliwa na akashuka Regna akiwa amevalia kama alivyo kuja kuniomba mara ya kwanza juu ya kuhitaji kuandika story ya kitabu kinacho husu maisha yangu
“Kaka Eddy, niagie kwa wifi yangu, na ile ishu ya story ninakuomba usisahau”
Regna alizungumza na kunifanya nibaki nikiwa nimemtazama kwa mshangao, nikashindwa hata cha kuwajibu
“Eddy, kaka Eddy”
Jamaa aliniita na kunifanya nistuke kwenye bumbuazi ambalo limenikamata gafla
“Yaaaa, sinto sahau”
“Sawa, ngoja sisi tukapumzike”
“Haya usiku mwema jamani”
Regna akanipungia mkono na kuingia ndani ya gari, wakaondoka na mume wake, nikashusha pumzi nyingi na kubaki nikiwa ninaisindikiza gari yao kwa macho hadi inatoka getini, gafla nikasikia kelele kubwa iliyo nistua na kunifanya nigeuke kuangalia walipo watu, nikawashuhudia wageni waalikwa wakikimbilia ndani inapo tokea kelele hiyo
Na mimi nikaanza kuchanganya miguu yangu kwa kasi kwenda kutazama ni kitu gani kinacho endelea ndani ya nyumba yangu.Jinsi ninavyozidi kwenda ndani ndivyo jinsi kelele ilivyozidi kuingia kwenye masikio yangu, nikazidi kuchanganyikiwa kwani kelele hiyo ni sauti ya Rahma ikitokea kwenye chumba ambacho nimemuacha na maiti, nikakuta watu wakiwa wamekushanyika nje ya mlango wa chumba nilicho muacha Rahma,
Nikawaomba wanipishe njia, na wakafanyahivyo hadi nikafika kwenye mlango, nikaanza kugongwa kwa nguvu ulu nikiliita jina la Rahma, gafla moshi mwingi ukaanza kutoka chini ya mlango, ulio anza kutupalia watu wote tuliopo kwenye eneo hili la mlango
Post your Comment