Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 75 na 76 )

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 75 na 76 )

Written By Bigie on Tuesday, April 3, 2018 | 4:44:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA-
0657072588 

ILIPOISHIA   
Nilipo hisi ninaweza kufa kwa kumwagiwa maji haya yenye nguvu, nikajigeuza na tumbu langu nikalielekezea kwenye ukuta, nikawaachia mgongo ambao wakaendelea kuushambulia kwa maji hayo nyenye nguvu hadi nikaishia wanguvu kabisa na kujikuta nikilala chini. Walipo niona nimelegea kabisa, wakanicha na kuufunga mlango wa chumba hichi cheye maji mengi na kunifanya nilale hapa chini huku machozi yakinimwagika na kujiuliza ni kitu gani kinacho endelea kwneye maisha yangu ya hivi sasa.

ENDELEA
Taratibu nikajinyanyua huku mwili wangu ukiwa umejawa na maumivu makli sana yaliyo tokana na kumwagiwa maji yenye nguvu. Nijajarubu kusimama ila mwili mzima ukakosa nguvu, sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kukaa hapa chini. Haukupita muda mwingi, mlango ukafunguliwa wakaingia wasichana wanne ambao  ni tofauti kabisa na wale ambao walinimwagia maji. Wasichana hawa ambao miili yao imejengeka kwa misuli kama wanaume, wakanifwata na kuninyanyua, wakaanza kuniburuza
na kunitoa nje ya chumba hichi.

Wakanipitisha katika kordo ambayo ina vyumba vingi vya wafungwa na vina mageti ya vyuma. Karibia wafungwa wote ambao wapo ndani ya vyumba vyao waliendelea kunitazama kwa umakini huku wengi wao wakionekana kunikasirikia sana. Mlango wa chumba kimoja ukafunguliwa. Wakanisukumia ndani ya chumba hichi chenye hewa nzito sana. Nikaanguka  chini huku nikiwa nina hema sana. Nikastukia nikiwa nimeguswa mgongoni, taratibu nika na kumtazama aliye nishika. Nikakuta ni yule kijana wa kiharabu ambaye alinikaribisha katika kiti cha pembeni alicho kuwa amekikaa.
”Pole”
Alizungumza huku  akinitazama usoni mwangu, taratibu akanipa mkono wake, akaninyanyua huku akinitazama usoni mwangu. Taratibu akanisaidia kunikalisha kitandani, nikakitazama chumba hichi chenye vitanda viwili ambavyo vina vitanda vya juu na chini ambavyo vijajulikana kwa jina la double deka. 
 
“Hivi hapa ni wapi?”
Niliuliza huku nikihema sana.
“Kusema kweli mimi bado sijaelewa hili eneo, mimi nilitekwa tu na kujikuta nikiwa humu ndani ya hili gereza”
“Una muda gani hadi kuwemo kwenye hili gereza?”
“Ni mwaka sasa, ni siku nyingi sana nimetekwa, sifahamu kama familia yangu ina hali gani?”
“Na kwenye hichi chumba unaishi na nani?”
“Tulikuwa watatu, ila wawili wamesha kufa kwenye yale mapambano kwenye ule ulingo. Yaani hili gereza kwa haraka haraka hii ni sehemu ya kifo, mtu anaingia ila hakuna ambaye anaweza kutoka”
Taratibu nikashusha pumzi huku nikiutazama mlango ulio tengenezwa na nondo. Kusema kweli nilisha ingia kwneye magereza kadhaa kama mtembezi, hata gereza nililo kuwa nimefungwa miezi kazaa iliyo pita lina nafuu tena kubwa sana, kwa maana nilifungiwa tu kwenye chumba kimoja ila hili lina mchanganyiko mkubwa wa watu wa kila aina na karibia asilimia tisini na tisa ya watu wa humu ndani ya hili gereza wana roho mbaya sana.
 
“Hili gereza lina mateso sana. Kwa siku milo ni mara mbili, asubuhi na jioni. Wenye nguvu ndio wanakula, ila sisi wanyonge ndio tunao shinda njaa”
Kijana huyu wa kiarubu alizungumza huku akiwa katika hali ya unyonge sana.
“Unaitwa nani?”
“Ahmood wewe je?”
“Dany”
“Unatokea nchi gani?”
“Tanzania”
“Mimi ninatokea India”
“Ahaaa”
“Hivi munajuaje kama sasa hivi ni usiku au mchana?”
“Hakuna anaye fahamu kwa kweli, sisi tunaishi kwa masaa, kengele ya kuamka ikipigwa, sisi tunaamka, kengele ya chakula ikipigwa sisi tuna kwenda sehemu ya chakula. Kengele ya kulala ikipigwa sisi tunaelekea kulala”
 
“Ahaa kwahiyo hapa watu wanaishi kwa kengele?”
“Yaaa, ila kuna saa kwenye kila sehemu ya hili jengo, kwahiyo unaweza kuangalia saa kisha unaweza kuhesabu siku wewe mwenyewe”
“Hapo nimekuelewa, vipi mbona kuna mapambano ya maujia?”
“Kama nilivyo kuambia pale awali, hapa kuna mchezo ambao huwa unafanyika, na ni mchezo ambao kusema kweli unarushwa kwenye mtandao wao wa siri ambao watu huko huwa wanalipia pesa nyingi sana”
“Mchezo huo wa kuuana?”
“Ndio mchezo huo huo, mmiliki wa hili gereza huwa anajivunia mabilioni ya pesa kwa kila wiki, na kunakuwa na mechi zinazo anzia mtoano hadi mmoja anafika fainali na yule mshidi huwa anatolewa gerezani, ila hakuna anaye fahamu ukweli wa huyo mshindi huko uraiani anakwenda kufanya kitu gani”
 
Maneno ya Ahmood yakanifanya niweze kuelewa hili geraza kiuharaka kabisa, na nikatambua kwamba si gereza la kiserikali na inavyo onekana ni gereza la siri ambalo lipo kimaslai ya watu fulani kutokana na maisha ya watu.
“Mmiliki wa hili gereza unamtambua?”
“Hakuna anaye mfahamu mmiliki wa hili gereza, na sisi sote tunalindwa na hawa wasichana, huwa wana roho mbaya, kwao kukuua ni swala rahisi sana, ndio maana unaweza kuona mijitu na miili yao wanashindwa kuwadhuru hawa wasichana”
“Ahhaa na kuna wafungwa wa kike?”
“Hapana hakuna wafungwa wa kike, yaani humu ni wanaume tu na kila siku wafungwa wanazidi kuongezeka. Kwa mara ya kwanza ni ngumu sana kuweza kufahamu kam……”
Ahmood akaka kimya mara baada ya taa zote kuzimwa.
“Vipi?”
 
“Shiiiii”
Ahmood alizungumza huku kwa haraka akijilaza kitandani ikanibidi na mimi kuweza kufanya hivyo kwa mana hata minong’ono nilivyo kuwa nikiisikia katika vyumba vingine imenyamaza kimya kabisa. Nikatatamani kuuliza kitu ila nikaka kimya kwa maana mateso niliyo yapata kwa muda fulani yananitosha. Dakika na masaa yakazidi kukatika kukiwa kimya kabisa. Msongamano wa mawazo ya kufikiria vitu vilivyo tokea kwenye maisha yangu. Picha ya mwangu pamoja na Asma kwa mara kadhaa zikaendelea kujitokeza kwenye mfumo wangu wa mawazo, nikamfikiria mama yangu, mdogo wangu pamoja na baba yangu. Kusema kweli hali niliyo nayo sasa hivi sielewi nitaanzia wapi hadi niwe huru. Kwa uchovu na wingi wa mawazo nikajikuta nikipitiwa na usingizi na kulala fofofo.

Mlio wa kengele ukapigwa na kutufanya sote kuamka, nikakuta taa zote zikiwa zimewashwa. Miliango ikafunguliwa na wafungwa wote tukatoka. Ahmood akatangulia mbele yangu, nikamfwaya kwa nyume kuelekea wanapo kwenda wafungwa wengine wanao kimbia. Tukaingia kwenye moja ya kiwanja kikubwa na sote tukasimama kwenye mistari ambayo sikuweza kuihesabu kwa haraka haraka, ila mimi nikawa nyuma ya Ahmood. Tukaanza kuhesabiwa namba na wasichana hawa ambao wamazi yao ni ya kijeshi. Baada zoezi hilo kumalizika, tukatawanyika na kila mtu akawa huru.
“Sasa hapa tunafanyaje?”
 
“Hapa watu wanafanya mazoezi, baada ya hapo tunapata kifungua kinywa”
“Baada ya hapo?”
“Wao ndio wanapanga ratiba baada ya chai, kwa hiyo hakuna ratiba ambayo inajulikana baada ya kupana kifungua kinywa”
Mimi na Ahmood tukatafuta sehemu ambayo imetuli tukaa na kuwatazama wafungwa wengine wakiendelea kufanya mazoezi ya kunyanya vyuma huku wengine wakifanya mazoezi ya kuruka kamba. Kwa maumivu ambayo ninayo sina hata hamu ya kufanya zoezi jengine.
“Hawakukupa viatu jana?”
“Ndio”
“Utapatiwa, ila hakikisha kwamba namba yako uliyo pewa leo unaikumbuka, kwa maana hapa hatuitwi kwa majini ni namba tu”
 
“Ehee na  nilisha isahau”
“Wewe ni namba elfu moja tisini na sita”
“Asante kwa kunikumbusha kwa kweli.”
“Tanzania ulikuwa unafanya kazi gani?”
“Ahaa nilikuwa ni mwalimu tu”
Ilinibidi kuongopea kwa maana simuamini mtu yoyote kwenye maisha yangu kwa maana nina amini pasipo Livna kutugeuka mimi na Mariam wala sasa hivi nisinge kuwa kwenye maisha haya ambayo hayaeleweki kabisa.
“Ahaaa mimi nimesomea maswala ya Teknolojia, hapa maswala ya computer yamelala kichwani”
“Vizuri sana”
“Yaa muda mwengine huwa ninawasaidia wanapo kuwa wamekwama kwenye masala ya kimitandao”
“Na ofisi zao za kurushia hayo matangazo zipo wapi?”
“Sifahamu, huwa wakinichukua wananifunga kitambaa cheusi kwenye macho wananipelekea na nikimaliza kazi wananirudisha hivyo hivyo”
 
“Hukuwahi kutazama tazama kwenye mitandao yao na kufahamu kwamba tupo wapi?”
“Kaka huwezi kufanya hivyo kwa maana wanakusimamia kwa mitutu na kila hatua unayo pita kuna wasichana wanao shuhulika na maswala hayo wanakufwatilia”
“Ahaaa, haya mapambano yao wamafika hatua gani?”
“Wapo nusu fainali na kesho kutwa ni fainali. Baada ya hapo wananza msimu mwengine  na wasindani wanaweza kuwa hata mia moja, kwa maana kila mmoja anatamani kuondoka taika eneo hili”
Tukanyamaza kimya baada ya kumuona msichana mmoja
akitufwata sehemu tuliyipo. Akasimama mbele yetu.
“Namba elfu moja tisini na sita nifwate”
Nikanyanyuka na kuanza kumfwaya kwa nyuma. Tukaongozana na askari huyu huku nikiendelea kutazama maeneo ya gereza hili kwa umakini. Gereza hili kusema kweli ulinzi wake ni mkali sana kwa manaa kuna kameza nyingi kila sehemu na kameza zote zinarekodi matukio yote yanayo endelea katika eneo hili.
 
Tukaingia kwenye moja ya ofisi na kumkuta mwana mama mmoja aliye valia nguo zenye vyeo vya kijeshi akiwa amesimama nyuma ya meza yake iliyo jaa compyuta zaidi ya sita. Msichana aliye nileta akatoka na kuniacha na mwana mama huyu mwenye sura nzuri ya kuvutia ila ina alama kubwa ya kuchanwa na kitu chenye ncha kali kwenye shavu lake la upande wa kulia.
Akachukua rimoti iliyopo mezani, akawasha tv iliyopo kwenye ukuta, tukio la mimi kupambana na jamaa aliye nisukuma jana usiku likaanza kuonekana hadi likafikia hatua ya mimi kundolewa eneo la uwanja huo. Video hiyo ikaendelea kuonyesha matukio ya mimi kumwagiwa maji mengi na askari wake. Alipo maliza kunionyesha matukio hayo, akazima tv hivyo na kunikazia macho yake. Sikuona haja ya kutetemeka wala kuhofia chochote kwa maana maisha yangu yapo reheni kwa wakati huu kwani kifo muda wowote kinaweza kunichukua.
 
“Unafahamu ni hasara gani uliyo tupa kwa ugomvi wako?”
Nikabaki nikimshangaa sana huyu mama, si kwa uzuri wake au swali alilo niuliza, ila ninamshangaa kwa kuzungumza Kiswahili fasaha pasipo kukosea.
“Hasara gani?”
Niliuliza swali badala ya kumjibu swali alilo niuliza.
“Umevuruga Tv show yangu”
Mwana mama huyu alizungumza kwa sauti ya ukali huku akiwa amenikazia macho hadi kawaga kwa mbali kakaanza kuninyemelea ila nikajikaza nikiamini kwamba hata kama nipo kwenye gereza, ila nimesha jitolea kufa na kupona.
“Laiti kama jana ningekuwepo ningekikata kichwa chako kwa mkono wangu mimi mwenyewe. Unabahati sana na nilihitaji uachwe hadi mimi nije kukuoana”
 
“Kila unacho kizungumza mimi sikielewi, na huo ndio ukweli?”
“Ohoo huelewi?”
Mama huyo akachukua rimoti yake na kuisha Tv yake, akanionyesha maoni mfululizo yaliyo ingia kupitia mtandao wao walio anzisha kipindi chao hichi cha mauaji. Kila maoni ninayo soma yanaonyesha ni jinsi gani mashabiki walivyo kasirishwa na tukio ambalo lilijitokeza jana usiku
“Ninakupa machoguo mawili, kifo au kuingia ulingoni kuhakikisha unafuta hii aibu uliyo nipatia”
“Baada ya hapo?”
“Utaendelea kunitumikia mimi”
“Siwezi kuchagua chochote”
“Ahaa katika hili utachagua”
Mwanamama huyu akabadilisha video inayo onekana na kuniwekea video iliyo nifanya macho yanitokea huku taratibu mapigo yangu ya moyo yakianza kunienda mbio kiasi cha kuanza kulifanya jasho langu kuanza kunitiririka taratibu.
 AISIIIII……….U KILL ME 76                                                                                                   
     
Macho yangu yakamuona Mariam akiwa katika mateso makali, mwili wake mzima umejaa majeraha ya kuchanwa chanwa. Machozi yakaanza kunilenga lenga, uzuri wa Mariam wote umebadilika na kuwa mbaya.
“Maisha yake yanakutegemea wewe, ukiendelea kuwa mkaidia, basi anakwenda kufa na kifo chake kitakuwa mikononi mwako”
 
Mwanamama huyu alizungumza kwa msisitizo, kisha akazima tv yake na kunitazama usoni mwangu kwa macho yake yaliyo jaa ukali.
“Ni kitu gania kinacho endelea?”
“Hicho ulicho kiona hapo ndio kitu kinacho endelea. Hakikisha kwamba unafanya uchaguzi sahihi la sivyo mpenzi wako anakwenda kufa. Walinzi njooni”
Mwana mama huyo alizungumza, mlango ukafunguliwa wakaingia wasichana wawili na kunitoa ndani ya hii ofisi. Wakanisindikiza hadi sehemu nilipo muacha Ahmood nikamkuta akiwa amezungukwa na majamaa wanne, ambao walipo tuona mimi na hawa askari wakanyamaza kimya. Wasichana hawa wakaniacha na kuondoka zao nikabaki peke yangu. Nikawatazama majamaha hawa, mmoja wao nikamuona akiwa ameshika kisu kidogo na wanavyo onekana walikuwa wakimuonea Ahmood.
 
Sikutaka kuwasemesha chochote zaidi ya kuwapita na kukaa pembeni ya Ahmood ambaye sura yake imepoteza kabisa furaha.
“Wanahitaji nini hawa majamaa?”   
“Wanhitaji haki yao”
“Haki yao?”
“Ehee”
Ahmood alizungumza kwa woga sana, kitu ambacho ninajiuliza hi haki gani ambayo watu hawa anaihitaji kutoka kwa Ahmood.
“Ni haki gani?”   
Ahamood akaka kimya huku akitetemeka, jamaa mmoja akamshika mkono Ahmood na kuhitaji kumvuta kwa upande wake ila nikauwahi kuuvuta mkono wa Ahmood na kumzuia kuto kuvutwa na jamaa huyo.

Jamaa niliye mkatalia kumvuta Ahmood akajaribu kunivamia ila nikawahi kumrudisha alipo toka kwa teke la kifua, lililo mfanya kuanguka chini kama mzigo na kuwafanya wezake kumuangalia. Nikasimama wima huku nikiwatazama kwa macho ya ukali sana. Wezake wote wakaonekana kusita katika kunivamia, naamini swali wanalo jiuliza watu wengi ni kitu gani kinacho nifanya kujiamini kwa kiasi kikubwa isitoshe mimi ni mgeni. 

Mwenzao aliye anguka chini anaye tafuta jinsi ya kunyanyuka, akaanza kuwapa amri wezake kwa ishara ya kunivamia, hapo ndipo nikagundua kwamba huyu niliye mpiga ni mkubwa wao na wanamuogopa kwa maana hata kuvamia kwao wanakuja kwa kujishauri sana. Wakajaribu kuonyesha ujuzi wao katika kupigana ila kusema kweli hawana mbinu yoyote ambayo inawawezesha wao kupigana na mimi. Kila aliye nifwata niliweza kumuhimili na kitu kikibwa nilicho jitahidi ni kuhakikisha hakuna hata mmoja anaye weza kunigusa kwa ngumi wala teke.

Wafungwa ambao  walikuwa wanafanya mazoezi, waliyasitisha kwanza mazoezi yao na kututazama jinsi tunavyo parangana. Hata Ahmood naye yupo pembeni amejikausha kimya akitazama jinsi ninavyo watembezea wezake kipigo kikali. Kitu kilicho nishangaza sikusikia king’ora wala ishara yoyote kutoka kwa askari hawa wa kike wanao tulinda na sehemu tuliyopo tunaonekana kabisa kwa maana wapo wengi wamesimama maeneo ya juu wakiwa na silaha zao wakizunguka kutoka upande mmoja kwenda nyingine. Watu hawa ambao walipanga kumletea fujo Ahmood wote wakawa chini wamelala kila mmoaj akiugulia sehemu yake kwa maana, nimejitahidi kuhakikisha ninawapiga sehemu ambazo hakuna anaye weza kuendelea kupambana na mimi.

Ukimya ukatawala katika eneo zima, wafungwa zaidi ya elfu tano wamebaki wakiwa wamesimama wakiniangali. Sauti ya makofi ikasikika kutoka nyuma yangu, ikanibidi kugeuka. Nikamkuta mzee mwenye asili ya Kijapani ndio anaye piga makofi. Taratibu akanisogelea hadi sehemu nilipo simama huku akiwa na tabasamu pana usoni mwake, akatingisha kichwa huku akinishika kwenye bega langu. Akanitazama tena na kunipa mkono, taratibu nikampa mkono, akautingisha mkono wangu kwa nguvu, ila nikauwahi kuukaza.  Akazungumza maneno kadhaa huku akimtazama Ahmood.
“Anasema hongera sana kwa kazi uliyo ifanya”
Ahmood alinitafsiria kwa manaa lugha aliyo izungumza sikuielewa.
“Muambie asante”
Ahmood akazungumza na mzee huyo. Kisha mzee huyo naye akazungumza na Ahmood akanitafsiria tena.
“Anakuambia kama huto jali anahitaji kukufanya kuwa bora zaidi ya hapo”
“Kivipi?”
“Yaani akufundisha mapigo mengine mapya ya kupambana yatakayo kufanya kuwa bora”
 
“Sawa mimi sina tatizo”
“Kingine amesema anahitaji ujiunge kwenye timu yake”
“Kwani humu ndani kuna kuwa na timu?”
“Yaa zipo timu, sema huyu mzee amebakiwa na kijana mmoja ambaye naye ameingia nusu fainali, vijana wake wengine wote wamesha uwawa kwenye mapambano”
“Mmmm, nitajiunga”
“Amekuambia kesho asubuhi, nikupeleke kwenye sehemu yake ya mafunzo”
“Sawa”
Baada ya kuzungumza na mzee huyu, akandoka, wafungwa wengine wakaendelea na mazoezi yao, mimi na Ahmood tukaondoka eneo hili, akaanza kunitembeza kwenye maeneo ya hili gereza, huku akinionyesha sehemu mbali mbali ambazo wafunga tunaruhusiwa kupita. Kila sehemu ambayo ninapitishwa nikahakikisha kwamba ninaiweka kichwani mwangu, wazo la kutoroka bado lipo pale pale na maswala ya kutamani kufa nikayafuta kabisa akilini mwangu.

Kusema kweli hili gereza linatisha, kuanzia ulinzi hadi muonekano wake. Ni geraza ambalo halina jina kabisa, wala halina sehemu ambayo kunaingia mwanga wa jua. Kila sehemu kuna taa kubwa nyingi sana zenye kulifanya eneo zima kuwa kama mchana. Wanajeshi wa kike wapo wengi sana, wamechanganyikana wa asili tofauti tofauti kwa maana wapo wafrika, wazungu na watu wa bara la Asia. Kila sehemu ya hili gareza kuna vipaza sauti vinayo wezesha wafungwa wote kusikia kila kitu kitakacho tokea hususani kengele za kutoa ishara tofauti.
   
Kengele ya kupata kifungua kinywa ikagonga, tukaongozana na Ahmood hadi kwenye holi  la kupatia chakula, ambapo tukakuta wafungwa wengine wakiwa wamesha panga mistari kwa ajili ya kwenda kupata chakula. Tukatafuta msari ambao hauna wafungwa wengi na sisi tukasimama. Macho yangu yakendelea kuchunguza hili eneo kwa maana kwangu ni jipya. Wapakuaji wa chukula ni wanajeshi hawa wa kike.
“Maisha haya yananikumbusha kipindi nikiwa shuleni”
“Mulikuwa munakula kwa kupanga mistari kama hapa?”
“Yaa tena kwa kengele kama hapa tu, sema kuna utofauti. Hapa ni gerezani na kule ni shule”
“Kweli, huwa ninasikia kwamba Tanzania ni inchi ya amani sana?”
 
“Yaa ni nchi ya Amni, japo kuna mambo mengi yanajitokeza ya hapa na pale. Ila ndio hivyo tunayavumilia kibishi bishi”
Hadi ninamalizia kuzungumza sentensi hiyo, tukawa tumesha fika karibu kabisa na mpakuaji huyu wa kike mwenye nywele ndefu, na ni mrefu kiasi. Akanikazia macho sana, kutokana Ahmood yupo mbele yangu, ikanibidi niyakwepeshe macho yangu na kutazama pembeni kwenye sahani. Nikachukua sahani na kikombe changu kisha nikasubiria Ahmood kupakuliwa chakula chake na mimi nikasogea mbele. Nikanyoosha sahani yangu, ila huyu mpishi akaendelea kunikazia macho hadi nikasita kidogo na kuirudisha sahani yangu nyuma kidogo.
 
“Weka sahani yako vizuri”
Msichana huyu alizungumza Kiswahili na  kunifanya nimkazie macho na mimi, nikaiweka vizuri sahani yangu, akaniwekea vipande vya mikate viwili na kipande cha soseji, akanimiminia chai kidogo na nikaondoka katika eneo hili, huku nikijaribu kutazama tazama nyuma kumuangalia dada huyu aliye nipakulia chukua.

Nikafika katika sehemu aliyo Ahmood na mimi nikaka na kuanza kula taratibu. Kitu kinacho nitesa kwa wakati huu ni ubaridi ninao upata kwenye nyayo zangu, kutokana na holi hili limesakafiwa na simenti inayo hifadhi ubaridi mkali sana. Nikainyanyanyua miguu yangu juu kidogo, nikageuza macho yangu sehemu watu wanapo pakuliwa chukula. Macho yangu yakakutana uso kwa uso na msichana aliye nipakulia chukula.
“Vipi mbona yule dada anakutazama sana?”
“Hata mimi sifahamu ni kwanini ananitazama sana”
“Kuwa makini sana kwa maana humu ndani ikijulikana kwamba msichana mmoja ana mahusiano ya kimapenzi na mfungwa basi wanakuua, na msichan huyo anauwawa pia.”
“Mmmmm”
“Ahaa wee acha tu, usione hawa wasichana wakikatiza katiza, nao pia wana nyege, ila sheria ndio zinabana na sijui wamelambishwa dawa gani kwa maana ni wagumu na wana roho mbaya dhidi ya wanaume”
“Ngoja niangalie ana lengo gani kwangu”
 
Tukaendelea kula hadi tukamaliza, kwa siku ya leo wafungwa hatukupangiwa ratiba yoyote zaidi ya watu kuwa huru katika kufanya kazi binafsi, wapo walio safisha vyumba vyao, wapo walio fua nguo zao. Mimi na Ahmod tukatafuta sehemu tukaka na kuendelea kuzungumza mazungomzo ya maisha yatu ya urainani huko tulipo toka.
“Hivi unafahamu kwamba baba yangu ni waziri mkuu nchini India”
“Weee”
“Haki ya Mungu, baba yangu ni waziri mkuu, ila hadi sasa hivi sifahamu ni hatua gani ameichukua katika kunitafuta.”
“Hivi india muna raisi?”
“India mamlaka makubwa anayo waziri mkuu, kule mawaziri wetu wanachaguliwa na wananchi.”
“Ahaa”
“Ahaa wewe je, familia yako ipo vipi?”
“Mimi familia yangu ni ya kawaida sana, tunamaisha ya chini sana, kajikazi kangu ka ualimu ndio kidogo kalinifanya niweze kuiendesha familia yangu. Sasa hivi sipo sipati picha ni ugumu gani wanao upitia huko nyumbani”
 
“Pole sana Dany ila ukijitahidi unaweza kutoka, ila sisi wanyonge ndio tutafia humu ndani”
“Usijali tukisaidia nitahakikisha tunatoka pamoja humu ndani”
“Kweli Dany?”
“Yaa”
“Yaani ukinisaidia nikitoka humu ndani nitahakikisha kwamba ninakupa nusu ya utajiri wangu ambao baba yangu alisha nirithisha tangu utotoni”
“Sawa, hivi wale jamaa walio kuwa wanadai haki yao, ni haki gani huwa wanaitaka kutoka kwako?”
Swali langu likamfanya Ahmood kukaa kimya huku akinitazama usoni mwangu. Machozi yakaanza kumlenga lenga jambo lililo nifanya kidogo nimshangae.
“Niambie usilie”
Nilizungumza kwa sauti ya upole sana huku nikimtazama Ahmood. Akaka kimya akavuta makamasi ndani kidogo kisha akazungumza.
 
“Huwa wana……wana niingilia kinyume na maumbile kila siku”
Maneno ya Ahmood yakanifanya sura yangu niikunje kwa hasira hadi Ahmood akaogopa, katika maisha yangu huwa siwapendi wanaume wanao ingiliwa kinyume na maumibile.
“Huwa wananilazimisha na siku nyingine wanishikia kisu kunitishia kuniua pale tu ninapokuwa ninakataa wao kuningilia kimwili. Uwepo wako jana ya chumba changu, ndio nimelala kwa amani”
“Kwa hiyo wao ndio walio kuanzishisa huo umchezo na haukuwa nao tangia hapo nyuma?”
“Ndio”
Ahmood alinijubu kwa unyonge, nikasimama wima na nikamuamrisha tuanze kuwasaka wale walio mfanyia mchezo huo mchafu. Ahmood hakuwa na kipingamizi kwa maana sura yangu imejikunja kwa hasira. Tukaanza kuzunguka maeneo tofauti tofauti ya hili gereza, kutokana sura ninazikumbuka vizuri sikuwa na wasiwasi katika kuwatafuta. Karibi robo tatu ya gereza tukalimaliza ila hatukuwaona.
 
“Unafahamu ratiba zao?”
“Hapana”
“Huwezi  kuhisi labda wanweza kuwa wapi kwa muda huu?”
“Sifahamu, ila twende kwenye mabafu”
Tukaongozana na Ahmood hadi kwenye mabafu na kweli, tukamkuta kiongozi wao akioga peke yake. Alipo tuona mimi na Ahmood wasiwasi mwingi ukamjaa akatamani kukimbia ila kwa bahati mbaya katika bafu hilo hakuna mlango wa kutokea.
“Inama”
Nilimuamrisha jamaa huyu, ila akaonekana haielewi lugha ninayo izungumza. Ahmood akabaki amekodoa macho, kwa nguvu nikamshika shingo jamaa huyu na kumuinamisha na kumfanya abong’oe na kuyaacha makalio yake yaeleke kwa Ahmood.
“Ahmood vuo nguo zako na wewe uwafanye kama kile walicho kifanya wewe”
Maneno yangu yakazidi kumshangaza kwani hakutegemea kabisa kama ninaweza kulifanya tukio hilo. Nikakazia macho Ahmood ambaye naye kwa woga akaanza kuvua suruali yake haraka haraka ili kufanya kile ambacho ninamuambia akifanye.
                                                                            ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts