CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa wito kwa wanafunzi kutoka vyuo vikuu kugombea nafasi za uongozi serikalini, kuanzia ngazi za vijiji ili kufikisha elimu ya mabadiliko kifikra maeneo hayo.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa tawi la Chadema Chuo Kikuu cha Mtakatifu John, tawi la Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa (Bavicha), John Heche, alisema wananchi wengi vijijini wanakabiliwa na matatizo mengi ya umaskini yanayotokana na ukosefu wa uongozi bora.
“Tanzania ina zaidi ya vijiji 20,000 maeneo hayo yote Dk Willibrod Slaa hawezi kuyafikia na akitaka kufanya hivyo itamchukua muda mrefu, ninyi mliopata elimu ndiyo mnaostahili kwenda huko na njia pekee ya kuleta mabadiliko ni kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi za vijiji,” alisema Heche.
Heche alisema kwa sababu hivi sasa chama kina mtandao kila chuo kikuu cha Tanzania, njia hiyo ndiyo itakayowezesha wananchi kunufaika na elimu ya vijana kutoka vyuo vikuu.
Katika hatua nyingine, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Dk Kitila Mkumbo, alikabidhi kadi kwa wanachama wapya 56 kutoka Chuo cha Mtakatifu John, akiwamo Mhadhiri wa chuo hicho, Martine Tetti.
Dk Mkumbo alisema unahitajika ujasiri katika kutekeleza dhana ya mabadiliko nchini, kwa kuwa CCM imekuwa ikitumia mbinu mbalimbali za kutaka wasomi wasihusike kwenye siasa ili kuendeleza siasa chafu za ufisadi na rushwa.

Post your Comment