Dk. Makongoro Mahanga
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo inatarajiwa kutegua kitendawili cha ama kuthibitisha au kubatilisha matokeo ya ubunge wa Segerea yaliyompa ushindi, Dk Makongoro Mahanga.
Kesi hiyo namba 98 ya mwaka 2010, itasomwa leo na Jaji Profesa Ibrahimu Juma ambaye amekuwa akiisikiliza tangu ilipofunguliwa Novemba 10, 2010.
Kesi hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo kupitia Chadema, Fred Mpendazoe akipinga ushindi wa Dk Mahanga wa CCM akidai kuwa sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi zilikiukwa katika hatua ya kuhesabu, kujumlisha kura na kutangaza matokeo.
Kutokana na dosari hizo, Mpendazoe ambaye amekuwa akiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala, aliiomba Mahakama itengue matokeo hayo na iamuru uitishwe uchaguzi mwingine mdogo katika jimbo hilo au imtangaze yeye kuwa mshindi akidai kwamba alipata jumla ya kura 56,962 na Mahanga kura 44,904.
Mbali na Dk Mahanga ambaye ni mdaiwa wa pili katika kesi hiyo, mdaiwa wa kwanza ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na wa tatu ni Msimamizi wa Uchaguzi (RO), katika jimbo hilo.
Dk Mahanga amekuwa akitetewa na Mawakili Jerome Msemwa na Aliko Mwamanenge na AG na RO wamekuwa wakitetewa na Mawakili wa Serikali, David Kakwaya na Seth Mkemwa.
Wakati wa ushahidi wake, upande wa madai uliwaita mahakamani mashahidi 13 akiwemo mlalamikaji mwenyewe Mpendazoe na wadaiwa wote watatu kwa pamoja waliwaita jumla ya mashahidi 16.
Mpendazoe katika hati yake ya madai alidai kuwa fomu za matokeo ya kura katika baadhi ya vituo katika Kata za Kiwalani na Vingunguti zilipotea na matokeo hayo hayakujumlishwa katika matokeo ya jumla.
Pia alidai kuwa Dk Mahanga alikamatwa na masanduku ya kura na Mtendaji wa Kata ya Tabata , Imelda Kafanabo alikamatwa na fomu bandia na kwamba alighushi fomu za matokeo namba 21B na alifunguliwa mashtaka katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam na kijana mmoja alikamatwa na mihuri ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).
Sambamba na madai hayo, Mpendazoe pia aliwasilisha kielelezo kimoja mahakamani kama sehemu ya ushahidi wake, ambacho ni Gazeti la Mwananchi, la Novemba 2, 2010.
Gazeti hilo linaelezea kuwepo kwa mgombea wa ubunge katika jimbo hilo aliyekamatwa na masanduku ya kura Tabata Kimanga, huku habari hiyo ikileza kuwa jina la mgombea huyo na chama chake yanahifadhiwa.
Hata hivyo, Mashahidi kadhaa wa upande wa wadaiwa wakiwemo Dk Mahanga na AG, walikana madai yote ya Mpendazoe huku wakisisitiza kuwa uchaguzi huo ulizingatia taratibu zote.
Licha ya kukiri kusikia habari za mgombea kukamatwa na masanduku, Dk Mahanga alidai kuwa hakumjua huku RO naye akikana madai ya kwamba alikiri kusikia tukio hilo na kuahidi kulifanyia kazi.
RO alidai kuwa hata kama ingekuwa kweli kwamba mgombea huyo alikamatwa na masanduku, hayo yasingeweza kuathiri matokeo kwa kuwa yalikuwa na kura zilizokuwa zimeshahesabiwa.
Alidai kuwa cha muhimu kilikuwa ni fomu namba 21B, ambayo ndiyo iliyokuwa na matokeo ya wagombea wote kutoka katika vituo mbalimbali.
Aliongeza kuwa matokeo halisi ni yale yanayoonyeshwa kwenye fomu namba 24B, ambayo aliituma Nec yakionyesha kuwa Dk Mahanga alipata kura 43,554 na Mpendazoe kura 39,150.
Shahidi wa nne, aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Buguruni ilikodaiwa kuwa ndiko Dk Mahanga alikofikishwa na masanduku ya kura, alikana kuwepo kwa tukio hilo na kutaka mwenye ushahidi ikiwemo RB namba ya tukio hilo aiwasilishe mahakamani.
Kuhusu kupotea kwa fomu za matokeo Kiwalani na Vingunguti, waliokuwa wasimamizi wa uchaguzi wa kata hizo (AROs), walikanusha huku wakiwasilisha mahakamani fomu za matokeo ya vituo vyote hivyo kama vielelezo vya ushahidi wao.
RO na Dk Mahanga walipinga madai kwamba matokeo ya jimbo hilo hayakujumlishwa kwa mujibu wa sheria wakidai kuwa Mpendazoe hakuwemo katika chumba cha majumuisho, baada ya kugoma kuingia na wafuasi wake.
Kuhusu madai ya Mtendaji wa Kata ya Tabata, kukamatwa na fomu za matokeo ambazo zilidaiwa kuwa ni ya kupika, mtendaji huyo na RO walidai kuwa fomu hiyo ilikuwa ni ya matokeo ya udiwani ambayo ilikuwa imesahaulika ofisini.
Hoja 11 zilizokubaliwa
Kutokana na madai hayo, kabla ya kuanza kusikilizwa, mawakili wa pande zote mbili walikutana mbele ya Jaji na kuainisha mambo 11 waliyokubaliana kuwa ndiyo yanayobishaniwa ambayo yalipaswa kuthibitishwa.
Mambo hayo ni pamoja na kama mchakato wa kuhesabu kura, kujumlisha na kutangaza matokeo ya uchaguzi ulifanyika kwa mujibu wa sheria, kanuni na maelekezo ya kisheria.
Kama mchakato mzima wa uchaguzi ulikuwa huru wa haki na kwa mujibu wa sheria inayoongoza Uchaguzi Mkuu.
Kama mchakato wa kuhesabu matokeo ya vituo 120 vya Kata ya Kiwalani na 129 vya Kata ya Vingunguti na matumizi ya fomu ya matokeo namba 21B ulizingatia sheria.
Pia kama matokeo ya uchaguzi wa mbunge yalitangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi bila kuzingatia matokeo ta vituo 120 vya Kata ya Kiwalani na matokeo ya vituo 129 vya Kata ya Vingunguti.
Kama kuna mmoja aliyekamatwa na fomu ya matokeo namba 21B, mihuri ya Nec katika Kituo cha majumuisho ya kura za ubunge Anatoglou na alihojiwa na kufunguliwa mashtaka katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.
Kama masanduku saba ya kura yalikutwa yakiwa hayana lakiri na yaliathiri matokeo; Kama wakala wa mlalamikaji na wagombea wengine wa CUF na wa Sauti ya Umma (Sau) waliomba na wakanyimwa fomu za malalamiko kuwasilisha malalamiko yao juu ya kukosekana kwa fomu za matokeo kutoka Vingunguti, Buguruni na Kiwalani.
Kama jibu ni ndiyo katika hoja namba moja hadi nane, kama hayakukidhi kufikia kiwango kinachoelezewa na Sheria Uchaguzi ya Taifa na kama ni hivyo, ikiwa kutokukidhi huko kumeathiri matokeo ya uchaguzi.
Kama mlalamikaji alipata kura nyingi kama alivyodai katika hati yake ya marekebisho (aliyoiwasilisha Juni 20, 2011) na la mwisho ni mgombea yupi kwa mujibu wa fomu halali yanayothibitika, alistahili kutangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Segerea.

Post your Comment