
Diamond akiwa amevaa design ya Jokate
Msanii Diamond(jina kamili Naseeb Abdul), wikiendi hii anatarajiwa kuwa nje ya mipaka ya Tanzania wakati atakapopanda jukwaa kuburudisha wakati wa Live Eviction Show ya Big Brother Africa(BBA) huko Johanesburg, South Africa siku ya Jumapili saa mbili usiku kwa saa za Afrika ya Kati.
Diamond ambaye mapema mwaka huu aliongoza kwa kutwaa Tuzo za Kilimanjaro nchini Tanzania, ametangazwa hivi karibuni kuwemo katika orodha ya wasanii wanaowania tuzo za MTV African Music Awards(MAMA). Hongera Diamond!!
Advertisement
hapa