
Askari Polisi mmoja mkoani Kigoma mwenye namba D.1645 Stafu Sajenti S/SGT George Luzegama(53), ameuwa kwa kupigwa risasi na majambazi.Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SSP Francis Mwakabana, amesema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 3.30 usiku huko kwenye eneo la Mwanga Kitambwe mjini Kigoma ambapo majambazi yakiwa na sihala aina ya short Gun walimpiga risasi askari huyo mwenye namba D.1645 S/SGT George Luzegama(53).
Kamanda Mwaakabana amesema askari huyo alipigwa risasi kwenye mbavu za upande wa kushoto alipokuwa kwenye duka moja la madawa ambapo majambazi walikuwa wamevamia hapo na walimshambulia wakidhani ni miongoni mwa askari walioweka mtego wa kuwanasa.
Askari huyo alifariki muda mfupi mara baada ya kufikishwa wakiwa katika Hospitali ya Maweni mkoani Kigoma alipokuwa akipatiwa matibabu.Katika tukio hilo, majambazi hayo yalipora kiasi cha fedha za mauzo kutoka kwenye duka hilo na baadaye walikimbia kutokomea pasikojulikana na Polisi inaendelea na msako dhidi ya majambazi hayo
Post your Comment