Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » MASWALI YANAYODAI UFAFANUZI NA MAJIBU KUHUSU UHALALI WA BARAZA LA MAWAZIRI

MASWALI YANAYODAI UFAFANUZI NA MAJIBU KUHUSU UHALALI WA BARAZA LA MAWAZIRI

Written By mpekuaji on Sunday, May 6, 2012 | 3:28:00 AM

Kuna maswali kadhaa yanaulizwa katika mitandao mbalimbali ya mazungumzo na majadiliano kwenye intaneti.

Baadhi yanahitaji maelezo ya ufafanuzi na vifungu vya katiba kusimamia majibu hayo kikamilifu.

Yafuatayo ni mojawapo ya maswali hayo:

SWALI: Je, Wizara ya afya ni sehemu ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania? Ikiwa jibu siyo, je, chaguo la Dkt. Hussein Mwinyi
kuiongoza Wizara ya Afya kama Waziri si kukiuka sheria mama (Katiba)?

SWALI: Pamoja na kuwa Rais anayo mamlaka kwa mujibu wa sheria kuteua Wabunge 10, je ipo mamlaka katika Sheria Mama inayoruhusu kuteuliwa kuwa Waziri kabla kwanza ya kuapishwa kuwa Mbunge na kisha kuapishwa kuwa Waziri?

Yakiongezeka maswali mengine nitayaweka hapa.
Kazi ni kwako Mtanzania Mzalendo kusimamia sheria zinazokuhusu maamuzi ya maisha yako katika nchi yako!

Picture
Kombo Khamis Kombo
Katika kutafuta majibu, tovuti ya Bunge ina sehemu ya majibu kwenye swali la pili ambalo liliwahi kuulizwa Bungeni na Mbunge  Kombo Khamis Kombo  [CUF] tarehe 8 Juni 2011 lenye vipengele (a) na (b) kama ifuatavyo:

(a) Je, kuna Wizara ngapi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

(b) Je, ni Wizara ngapi zinahusiana na Mambo ya Muungano baina ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani?

Maswali hayo yalijibiwa na Mheshimiwa Suluhu, Samia Hassan wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Muungano: 

Samia Suluhu Hassan
Samia Suluhu Hassan
WAZIRI alijibu:- 

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kombo Khamis Kombo, Mbunge wa Mgogoni, lenye vipengele (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a)Idadi ya Wizara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikibadilika mara kwa mara kutokana na Rais anayekuwepo madarakani anavyoona inafaa kutekeleza kazi zake kulingana na mamlaka aliyopewa na Katiba. Kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Namba 494 la tarehe 17 Desemba, 2010 kwa sasa kuna Wizara 26 zinazoongwa na Mawaziri 29.

(b)Mheshimiwa Spika, jibu ni kwamba zipo jumla za Wizara 6 ambazo ni za Muungano, Wizara hizo ni Ofisi ya Makamu wa Rais inayoshughulika na Mambo ya Muungano, Wizara ya Fedha kupitia GFC, BOT na Sera za Kifedha, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Aidha, zipo Wizara ambazo si za Muungano lakini zinasimamia masuala ya Muungano kama yalivyoorodheshwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Mfano Wizara hizo ni Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambao hushughulika na suala la Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge ambayo husimamia masuala ya Bunge, Wizara ya Nishati na Madini ambayo husimamia suala la mafuta na gesi asilia, Wizara ya Katiba na Sheria ambayo husimamia suala la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Viwanda na Biashara ambao husimamia masuala ya Biashara za Nje, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia inayosimamia Masuala ya Mawasiliano, Wizara ya Uchukuzi ambayo husimamia suala la usafiri wa anga na majini na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambayo husimamia suala la Elimu ya Juu na Baraza la Mitihani la Taifa.

Soma zaidi: bunge.go.tz/bunge/parl_questions.php?memberid=1703 


ISEMAVYO KATIBA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - HAKI NA WAJIBU MUHIMU 

Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4 

21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria. 

(2) Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha yake au yanayolihusu Taifa. 

Haki ya Kufanya Kazi

Haki ya kufanya kazi Sheria ya 1984 Na.15 ib.6

22.-(1) Kila mtu anayo haki ya kufanya kazi. 

(2) Kila raia anastahili fursa na haki sawa, kwa masharti ya usawa, ya kushika nafasi yoyote ya kazi na shughuli yoyote iliyo chini ya Mamlaka ya Nchi. 

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts